title : MWAMBA WA HABARI YAPATA LESENI TCRA, YAJIPANGA KUFANYA MAKUBWA, YATOA OFA YA MATANGAZO SABASABA.
kiungo : MWAMBA WA HABARI YAPATA LESENI TCRA, YAJIPANGA KUFANYA MAKUBWA, YATOA OFA YA MATANGAZO SABASABA.
MWAMBA WA HABARI YAPATA LESENI TCRA, YAJIPANGA KUFANYA MAKUBWA, YATOA OFA YA MATANGAZO SABASABA.
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM.
Mwamba wa habari
Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo imetoa leseni kwa mtoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao wa intanenti Mwamba wa habari blog baada ya kutimiza vigezo.
Mwamba wa habari blog ni miongoni mwa blog zilizokizi vigezo na kupewa leseni kwa ajili ya kutoa huduma za maudhui kwa njia ya mtandao wa intanenti.
Akizungumza baada ya kupokea leseni hiyo Mkurugenzi wa Mwamba wa habari blog John Luhende,(Mwamba) amesema kuwa blog hiyo itaendelea kuuahabarisha umma kwa kuandika habari kwa zisizo na upendeleo zilizo zingatia uweledi katika tasnia ya habari.
Amesema kuwa ,wadau mbalimbali wanapaswa kuendelea kutoa ushirikiano kwa kuendelea kuiamini mwamba wa habari, kwani imejipanga kutoa habari makini kupitia vyanzo vya habari vya kuaminika na kupitia waandishi wake waliobobea katika tasnia ya uandishi wa habari.
"Tumejipanga kutoa huduma bora kwa wateja wetu, naomba wadau mbalimbali waendelea kutoa ushirikiano na kutuunga mkono" amesema Luhende.
Hata hivyo amebainisha kuwa katika kipindi hiki cha sabasaba ametoa OFA kwa taasisi na makampuni mbalimbali kuchangamkia fursa ya kujitangaza kwa bei nafuu.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa ametoa ofa hiyo ya matangazo kwa taasisi na wafanyabiashara kama sehemu ya mchango wake katika kuhakikisha Tanzania inafanikiwa katika kufanikisha uchumi wa viwanda.
Luhende amefafanua kuwa mawasiliano kwa njia ya mtandao kwa vyombo vya habari yanatakiwa kutumika vema ili kuwa na matumizi bora na salama.
Kwa upande wake Mhariri wa Mwamba wa habari Blog hiyo Noel Rukanuga, amesema blog inachapisha habari makini kwa kuzingatia maadili ya taaluma ya waandishi wa habari, jambo ambalo limefanya wasomaji wengi kupendelea kuisoma .
Amesema kuwa dawati lake la habari limejipanga kufanya kazi ili kuhakikisha kila wakati wanaendelea kutoa habari mbalimbali ikiwemo uchumi, biashara siasa pamoja na afya zenye vigezo kutoka ndani na nje ya nchi.
Rukanuga ambaye amewahi kufanya kazi katika magazeti mbalimbali ikiwemo gazeti la uchunguzi la Jamhuri, majira kwa miaka kadhaa, ameeleza kuwa kuongezeka kwa orodha ya blog zinazotambulika TCRA itakuwa chachu kwa blogger katika kufanya kazi kwa uhuru kwani wanatambulika kama chombo cha habari.
"Mfumo huu utasaidia kupunguza uanzishwaji holela wa vyombo vya habari mtandaoni usiokidhi viwango vinavyotakiwa katika kutoa habari, pia italeta ushindani na kutambua watu wenye nia safi ya kutoa huduma hiyo ya maudhui mtandaoni kwa jamii" amesema Rukanuga.
Hivyo makala MWAMBA WA HABARI YAPATA LESENI TCRA, YAJIPANGA KUFANYA MAKUBWA, YATOA OFA YA MATANGAZO SABASABA.
yaani makala yote MWAMBA WA HABARI YAPATA LESENI TCRA, YAJIPANGA KUFANYA MAKUBWA, YATOA OFA YA MATANGAZO SABASABA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MWAMBA WA HABARI YAPATA LESENI TCRA, YAJIPANGA KUFANYA MAKUBWA, YATOA OFA YA MATANGAZO SABASABA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/mwamba-wa-habari-yapata-leseni-tcra.html
0 Response to "MWAMBA WA HABARI YAPATA LESENI TCRA, YAJIPANGA KUFANYA MAKUBWA, YATOA OFA YA MATANGAZO SABASABA."
Post a Comment