TAFITI MBALIMBALI ZILIZOFANYWA NA WIZARA YA HABARI KUWASILISHWA KWA MAWAZIRI WA UTAMADUNI WA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA.

TAFITI MBALIMBALI ZILIZOFANYWA NA WIZARA YA HABARI KUWASILISHWA KWA MAWAZIRI WA UTAMADUNI WA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TAFITI MBALIMBALI ZILIZOFANYWA NA WIZARA YA HABARI KUWASILISHWA KWA MAWAZIRI WA UTAMADUNI WA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TAFITI MBALIMBALI ZILIZOFANYWA NA WIZARA YA HABARI KUWASILISHWA KWA MAWAZIRI WA UTAMADUNI WA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA.
kiungo : TAFITI MBALIMBALI ZILIZOFANYWA NA WIZARA YA HABARI KUWASILISHWA KWA MAWAZIRI WA UTAMADUNI WA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA.

soma pia


TAFITI MBALIMBALI ZILIZOFANYWA NA WIZARA YA HABARI KUWASILISHWA KWA MAWAZIRI WA UTAMADUNI WA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA.

Na Genofeva Matemu - WHUSM

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ameahidi kufikisha taarifa ya hatua ambayo Tanzania imefikia katika harakati za kutafiti na kuhifadhi kumbukumbu za ukombozi wa Bara la Afrika kwa mawaziri wa utamaduni wa nchi za kusini mwa Afrika ili nchi hizo wanachama ziweze kuendelea na hatua nyingine ya kuchangia katika ujenzi wa kituo cha kuhifadhi kumbukumbu hizo.

Waziri Mwakyembe ameyasema hayo leo Mkoani Mbeya alipofanya ziara kukagua maeneo yaliyotumika wakati wa harakati za ukombozi wa Bara la Afrika na kusema kuwa serikali ipo katika mpango ambao maeneo yaliyotumika katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika yatakarabati na kurejesha muonekano wake wa awali ili yasipotezi historia.

“Majengo yaliyotumika katika harakati za urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika ni sehemu ya historia na maeneo muhimu sana ambayo yanatakiwa kuboreshwa ili yaweze kuendelea kuwepo katika muonekano ule ule wa awali kwa lengo la kutokupoteza historia yake” amesema Mhe. Mwakyembe
Aidha Mhe. Mwakyembe amesema kuwa serikali imechukua wajibu wake wa kubaini maeneo yaliyotumika wakati wa harakati za ukombozi wa Bara la Afrika na kuwaomba viongozi wote nchi nzima kuendelea kubaini maeneo na vitu vilivyotumika katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika vilivyopo katika maeneo yao ili wizara   iyaendeleze kwa maslahi ya taifa na Afrika kwa ujumla.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Paul Ntinika (kulia) wakati wa ziara yake leo Mkoani Mbeya kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto mwenye miwani) akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Paul Ntinika (kulia mwenye miwani ) alipotembelea eneo la Game lililotumika kama kambi ya wapigania uhuru wa Msumbiji leo Mkoani Mbeya wakati wa ziara yake kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika

Nyumba zilizopo katika eneo la Game zilizotumiwa na wapigania uhuru wa Msumbiji ambazo kwa sasa zinatumiwa na Idara ya Maliasili na utalii. 

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akimsikiliza Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Bibi. Ingiahedi Mduma (kulia) alipotembelea Nyumba ya Binti Matola aliyekuwa mwanaharakati na rafiki wa Mwalimu Nyerere ambaye aliweza kumhifadhi Hayati Mwalimu Nyerere wakati wa kupigania uhuru wakati wa ziara yake kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika leo Mkoani Mbeya.


Hivyo makala TAFITI MBALIMBALI ZILIZOFANYWA NA WIZARA YA HABARI KUWASILISHWA KWA MAWAZIRI WA UTAMADUNI WA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA.

yaani makala yote TAFITI MBALIMBALI ZILIZOFANYWA NA WIZARA YA HABARI KUWASILISHWA KWA MAWAZIRI WA UTAMADUNI WA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TAFITI MBALIMBALI ZILIZOFANYWA NA WIZARA YA HABARI KUWASILISHWA KWA MAWAZIRI WA UTAMADUNI WA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/tafiti-mbalimbali-zilizofanywa-na_20.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TAFITI MBALIMBALI ZILIZOFANYWA NA WIZARA YA HABARI KUWASILISHWA KWA MAWAZIRI WA UTAMADUNI WA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA."

Post a Comment