MVUA YALAZA WAKAZI WA GOBA NJE, DALADALA ZAONJA BARABARA YA MWENDO KASI DAR

MVUA YALAZA WAKAZI WA GOBA NJE, DALADALA ZAONJA BARABARA YA MWENDO KASI DAR - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MVUA YALAZA WAKAZI WA GOBA NJE, DALADALA ZAONJA BARABARA YA MWENDO KASI DAR, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MVUA YALAZA WAKAZI WA GOBA NJE, DALADALA ZAONJA BARABARA YA MWENDO KASI DAR
kiungo : MVUA YALAZA WAKAZI WA GOBA NJE, DALADALA ZAONJA BARABARA YA MWENDO KASI DAR

soma pia


MVUA YALAZA WAKAZI WA GOBA NJE, DALADALA ZAONJA BARABARA YA MWENDO KASI DAR


Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

MVUA za masika zinazoendelea kunyesha katika Jiji la Dar es Salaam jana ziliacha watu njia panda baada ya daraja linalounganisha maeneo ya Goba, Tegeta na Madale kukatika na kusababisha adha kwa wakazi hao.

Mvua hizo zilianza kunyesha saa moja jioni hadi saa nne usiku ikiwa imeambatana na upepo mkali.Wakizungumza na Michuzi blog, leo jijini Dar es Salaam baadhi ya mashuhuda hao wamesema iliwalazimu kukesha katika maeneo hayo ili kulinda magari yao na wengine kutumia njia ya Tegeta A kufika majumbani kwao.

Aidha wakazi wengi walibaki maeneo hayo hadi saa saba usiku ambapo kivuko cha dharura kwa watembea kwa miguu kiliwekwa.Hadi asubuhi ya leo hali imeendelea kuwa tete kwani kivuko kilichopo kinawafaa watembea kwa miguu na pikipiki hali iliyoleta adha kwa wanafunzi wa Atlas Madale ambao imewalazimu kuchukua muda mrefu kufika shuleni.

Wakati hali ikiwa hivyo kwenye maeneo hayo,katika eneo la Jangwani Dar es Salaam zimebabisha daraja la eneo hilo maji kupita juu.Hali hiyo imesababisha usafiri kuwa mgumu kwa asubuhi ya leo kiasi cha mabasi ya mwendo kasi kusitisha kutoa huduma ya kusafirisha abiria.

Hivyo imesababisha kuwa na changamoto kwa wakazi ambao wanatumia usafiri huo.Hata hivyo taarifa iliyotufikia inaeleza kuwa huduma ya usafiri licha kusitishwa hatimaye imeanza na sasa mabasi hayo yanaendelea kutoa huduma.Athari za mvua zimesababisha kwa mara ya kwanza mabasi ya daladala za kutoka Mbagala-Kariakoo kuhamishiwa njia ya mbezi ili kusaidia kusafirisha abiria.

Na kubwa zaidi daladala hizo ziliruhusiwa kupita barabara ya mabasi ya mwendo kasi.Hata hivyo hali ya foleni katika barabara ya Morogoro haikuwa kubwa kutokana na njia nyingi ambazo magari yanaingia kwenye hiyo kutoka katika makazi ya watu nazo hazikuwa zinapitika.Hivyo kupunguza idadi ya gari ambazo zingeingia barabara hiyo.
 
HATA HIVYO.
 
 Kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam, UDA Rapid Transit (UDART), inapenda kuuujulisha umma kuwa, huduma za mabasi hayo zimerejea kuanzia saa 3:00 asubuhi tarehe 16/03/2018 baada ya kusitishwa kwa muda tangu saa 11:00 alfajiri kutokana kufungwa kwa Barabara ya Morogoro eneo la Jangwani kwa sababu ya mafuriko yaliyosababisha maji kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi. Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza. Deus Bugaywa, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART. 


Hivyo makala MVUA YALAZA WAKAZI WA GOBA NJE, DALADALA ZAONJA BARABARA YA MWENDO KASI DAR

yaani makala yote MVUA YALAZA WAKAZI WA GOBA NJE, DALADALA ZAONJA BARABARA YA MWENDO KASI DAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MVUA YALAZA WAKAZI WA GOBA NJE, DALADALA ZAONJA BARABARA YA MWENDO KASI DAR mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/mvua-yalaza-wakazi-wa-goba-nje-daladala.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MVUA YALAZA WAKAZI WA GOBA NJE, DALADALA ZAONJA BARABARA YA MWENDO KASI DAR"

Post a Comment