MAKUSANYO YA TRA YAVUKA TRILIONI 1 KWA MWEZI

MAKUSANYO YA TRA YAVUKA TRILIONI 1 KWA MWEZI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAKUSANYO YA TRA YAVUKA TRILIONI 1 KWA MWEZI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAKUSANYO YA TRA YAVUKA TRILIONI 1 KWA MWEZI
kiungo : MAKUSANYO YA TRA YAVUKA TRILIONI 1 KWA MWEZI

soma pia


MAKUSANYO YA TRA YAVUKA TRILIONI 1 KWA MWEZI

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kutoa taarifa ya makusanyo ya mapato ya kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/2018. Katika kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba 2017, TRA imekusanya jumla ya Shilingi Trilioni 3.65.

Makusanyo haya ni sawa na ukuaji wa asilimia 1.2 ikilinganishwa na makusanyo ya kipindi kama hicho kwa mwaka wa fedha 2016/17.

Katika kipindi hicho cha miezi mitatu, makusanyo ya kila mwezi yalikuwa kama ifuatavyo;-

Julai, 2017 Shilingi 1,101,193,417,551.91

Agosti, 2017 Shilingi 1,205,008,256,053.51

Septemba, 2017 Shilingi 1,345, 339,916,757.65
Kwa makusanyo haya, Mamlaka ya Mapato Tanzania, inapenda kuwashukuru wafanyabiashara na wananchi wote kwa ujumla kwa kuendelea kulipa kodi na kuiwezesha serikali kutimiza majukumu yake ya kuwahudumia wananchi.

Aidha, Mamlaka inapenda kuwakumbusha wafanyabiashara wote kutoa risiti za kielektroniki kwa kila mauzo na kudai risiti kwa kila manunuzi kwani ni njia pekee ya kupata mauzo sahihi yanayoiwezesha TRA kukokotoa kodi sahihi na kwa haki.

“Napenda kuwakumbusha wananchi wote kuhakiki risiti zao ili kuona usahihi wa tarehe na kiasi walicholipa na bidhaa waliyonunua kabla ya kuondoka na risiti hiyo. Endapo utaona haina vigezo tafadhali ripoti kwenye ofisi ya TRA iliyokaribu nawe au piga simu kituo chetu cha huduma kwa wateja kwa namba 0800750075 au 0800780078. anasisitiza Richard Kayombo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi

Vile vile, Mamlaka inawakumbusha wamiliki wa majengo nchini kulipa kodi ya majengo mapema badala ya kusubiri mwishoni mwa mwaka wa fedha ili kuepuka misongamano na usumbufu usio wa lazima.

Pia, wafanyabiashara wa michezo ya kubahatisha wanapewa wito wa kulipakodi zao kwa mujibu wa sheria ya michezo ya kubahatisha sura namba 41.
‘Pamoja Tunajenga Taifa Letu.



Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo akiongea na waandishi wa habari Dar es Salam leo Oktoba 10 2017 alipotoa takwimu za makusanyo ya zaidi ya Trilioni 1 kwa Mwezi kwa mamlaka hiyo kwa miezi ya Julai, Agosti na Septemba 2017. Pamoja naye afisa kodi Mkuu, Julius Ceaser.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo akiongea na waandishi wa habari Dar es Salam leo Oktoba 10 2017 alipotoa takwimu za makusanyo ya zaidi ya Trilioni 1 kwa Mwezi kwa mamlaka hiyo kwa miezi ya Julai, Agosti na Septemba 2017. Pamoja naye Maafisa kodi wakuu, Julius Ceaser (kushoto) na Sydney Mkamba.


Hivyo makala MAKUSANYO YA TRA YAVUKA TRILIONI 1 KWA MWEZI

yaani makala yote MAKUSANYO YA TRA YAVUKA TRILIONI 1 KWA MWEZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAKUSANYO YA TRA YAVUKA TRILIONI 1 KWA MWEZI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/makusanyo-ya-tra-yavuka-trilioni-1-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MAKUSANYO YA TRA YAVUKA TRILIONI 1 KWA MWEZI"

Post a Comment