title : Muhimbili Yapokea Msaada wa Vitanda na Magodoro
kiungo : Muhimbili Yapokea Msaada wa Vitanda na Magodoro
Muhimbili Yapokea Msaada wa Vitanda na Magodoro
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imepokea msaada wa vitanda 14, magodoro 12 pamoja na drip stands kutoka Australia Tanzania Society ambavyo vitasaida kuimarisha utoaji wa huduma hospitalini hapo.
Akipokea msada huo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Dkt. Juliethi Magandi amesema kwa muda mrefu hospitali imekua na ushirikiano na tasisi hiyo katika masuala mbalimbali ikiwemo kufanya upasuaji wa ubingwa wa juu.
“Kipekee nichukue fursa hii kuwashukuru rafiki zetu hawa Australia Tanzania Society kwa msaada huu walioutoa kwani tumekua tukishirikiana kwa zaidi ya miaka mitatu sasa,”. amesema Dkt. Magandi.
Amesema Hospitali ya Taifa Muhimbili ina jumla ya vitanda 1,507 na kwamba kina mama wajawazito na watoto pekee wanatumia karibu ya nusu ya vitanda hivyo. “Hivyo msaada huo umekuja wakati muafaka kwani hospitali bado ina mahitaji kutokana na kutoa huduma zake kila siku kwa saa 24,”.
Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Julieth Magandi akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kabla kukabidhiwa vitanda 14 na magodoro 12 ambayo yametolewa na Australia Tanzania Society. Kulia ni Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society, James Chialo na kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uuguzi na Mazingira Muhimbili, Zuhura Mawona.
Muuguzi Alice Msonda na Velena Joahackim wakitandika kitanda baada ya kukabidhiwa vitanda na magodoro na Australia Tanzania Society.
Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society, James Chialo akimkabidhi Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Muhimbili, Dkt. Julieth Magandi vitanda 14 leo. Katikati ni Mkuu wa Idara ya Uuguzi na Mazingira Muhimbili, Zuhura Mawona.
Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society, James Chialo akizungumza na waandishi wa habari leo kabla ya kukabidhi vitanda hivyo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Muhimbili Yapokea Msaada wa Vitanda na Magodoro
yaani makala yote Muhimbili Yapokea Msaada wa Vitanda na Magodoro Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Muhimbili Yapokea Msaada wa Vitanda na Magodoro mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/muhimbili-yapokea-msaada-wa-vitanda-na.html
0 Response to "Muhimbili Yapokea Msaada wa Vitanda na Magodoro"
Post a Comment