title : MAZIKO YA MZEE KWACHA YALIYOFANYIKA KIJIJI CHA PAJE LEO
kiungo : MAZIKO YA MZEE KWACHA YALIYOFANYIKA KIJIJI CHA PAJE LEO
MAZIKO YA MZEE KWACHA YALIYOFANYIKA KIJIJI CHA PAJE LEO
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’, ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Kada wake marehemu Mzee Abdulrazaq Mussa Simai 'Kwacha' aliyefariki leo Machi 11,20118.
Mzee Abdulrazaq amefariki katika Hospitali ya Kuu ya Taifa ya Muhimbili, iliyopo Jijini Dar es salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Katika Salamu hizo Dk. Mabodi amesema CCM imepokea taarifa ya kifo hicho kwa mshutuko mkubwa na uzuni ya hali ya juu, kutokana na marehemu Abdulrazaq alikuwa mwadilifu kwa Chama chake na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wote wa uhai wake, na amemtaja kuwa ni miongoni mwa Wana ASP aliyeyalinda na kuyathamini Mapinduzi ya mwaka 1964 kwa vitendo.
Kupitia salamu hizo Dk. Mabodi amewaomba familia ya marehemu, Wanachama, Viongozi na Watendaji wote wa CCM, Marafiki, Ndugu na Jamaa wote walioguswa na msiba huu kuwa na subra katika kipindi hiki kigumu na kuendelea kumuombea dua.
Enzi za uhai wake Abdulrazaq amewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika Chama na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ikiwemo Katibu Maalumu wa aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Aman Karume.
Marehemu amezikwa leo katika kijiji cha Paje wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja, amefariki akiwa na umri wa miaka 98 ameacha watoto watano na kizuka mmoja.Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu pahala Pema Peponi Amin.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali wakati alipowasili leo katika maziko ya MarehemuMzee Abdulrazak Mussa Simai (Kwacha) Mwanasiasa Mkongwe wa CCM katika Kijiji cha Paje Wilaya ya Kusini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kulia) alijumuika na Viongozi na Waislamu mbali mbali leo katika kumswalia Marehemu Mzee Abdulrazak Mussa Simai (Kwacha) Mwanasiasa Mkongwe wa CCM katika Msikiti wa Ijumaa Kijiji cha Paje Wilaya ya Kusini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akiweka udongo kaburini wakati wa maziko ya Mwanasiasa Mkongwe wa CCM Marehemu Mzee Abdulrazak Mussa Simai (Kwacha) baada ya kumswalia katika Msikiti wa Ijumaa Kijiji cha Paje Wilaya ya Kusini Unguja
Maelfu ya Wananchi kutoka sehemu mbali mbali za Zanzibar na Tanzania Bara walijumuika katika maziko ya Mwanasiasa Mkongwe wa CCM Marehemu Mzee Abdulrazak Mussa Simai (Kwacha) yaliyofanyika leo katika Kijiji cha Paje Wilaya ya Kusini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein ( kulia) alifika kuwapa mkono wa pole Wanafamilia ya Marehemu Mzee Abdulrazak Mussa Simai (Kwacha) Mwanasiasa Mkongwe wa CCM Nyumbani kwao baada ya mazishi yaliyofanyika leo katika Kijiji cha Paje Wilaya ya Kusini Unguja. Picha na Ikulu.
Hivyo makala MAZIKO YA MZEE KWACHA YALIYOFANYIKA KIJIJI CHA PAJE LEO
yaani makala yote MAZIKO YA MZEE KWACHA YALIYOFANYIKA KIJIJI CHA PAJE LEO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAZIKO YA MZEE KWACHA YALIYOFANYIKA KIJIJI CHA PAJE LEO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/maziko-ya-mzee-kwacha-yaliyofanyika.html
0 Response to "MAZIKO YA MZEE KWACHA YALIYOFANYIKA KIJIJI CHA PAJE LEO"
Post a Comment