title : Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), kuanza kuuza mananasi hai kutoka mkoani Njombe.
kiungo : Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), kuanza kuuza mananasi hai kutoka mkoani Njombe.
Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), kuanza kuuza mananasi hai kutoka mkoani Njombe.
Na Richard Mwaikenda
Tangazo la uuzaji wa mananasi limetolewa na Mkurugenzi Mtandaji wa Mkikita, Adam
Ngamange, ambaye hivi karibuni ameingia mkataba wa kuuza matunda hayo ndani na nje ya nchi.
Ngamange amewakaribisha Ofisi za Mkikita Dar es Salaam, wadau wenye maeneo ya kuuzia ili wapate utaratibu wa kununua jumla na kuyauza rejareja.
Bei ya mananasi hayo yaliyolimwa ki-organic kila moja huuzwa kwa bei ya kutupa ya sh. 1,200 itakayomwezesha muuza rejareja kupata faida kubwa.
Huduma hii inatarajiwa kuanza Machi 20 jijini Dar es Salaam, ambapo Mkikita imeingia mkataba wa kila wiki kuingiza sokoni nanasi 20,000.
"Hii ni fursa ya kuongeza kipato kwa wanaopenda kuwa wasambazaji na wenye mahoteli. Huu ndiyo mwanzo wa viwanda mkoani Njombe. Ungana na Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania kuhamasisha kilimo mkataba," amesema Ngamange.
Hivyo makala Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), kuanza kuuza mananasi hai kutoka mkoani Njombe.
yaani makala yote Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), kuanza kuuza mananasi hai kutoka mkoani Njombe. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), kuanza kuuza mananasi hai kutoka mkoani Njombe. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/mtandao-wa-kijani-kibichi-tanzania.html
0 Response to "Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), kuanza kuuza mananasi hai kutoka mkoani Njombe."
Post a Comment