title : MANGULA AONYA VIONGOZI WA DINI, WANASIASA WANOVURUGA AMANI NCHINI
kiungo : MANGULA AONYA VIONGOZI WA DINI, WANASIASA WANOVURUGA AMANI NCHINI
MANGULA AONYA VIONGOZI WA DINI, WANASIASA WANOVURUGA AMANI NCHINI
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Bara, Philipo Mangula amewataka Watanzania kujenga na kuilinda amani nchini na kushangazwa na viongozi wa dini wanaobariki chuki kuwa wanamkosea Mungu.
Pia aliwaonya wanasiasa wanaochochea chuki na kusababisha vurugu na kuwashauri waache kwa kuwa siasa ni uvumilivu na kuumiliana.
Mangula alitoa kauli hiyo jana mjini Musoma alipozungumza na viongozi na wana wana chama wa CCM kwenye ukumbi wa mikutano wa Chama mjini humo.
Alisema kuwa turufu kubwa iliyobaki kwa CCM na watanzania ni amani iliyodumu nchini kwa miaka dahari na hivyo wakati wote wazungumzie taratibu na kutunza amani ya nchi ili kue[uka machafuko vurugu na migogoro inayosababishwa na kuchochewa na wanasiasa.
“Siasa ni kuvumiliana na uvumilivu ndiyo hujenga umoja.Wanasiasa wanapoleta vurugu wajue wanaoumia ni watoto na wanawake na hivyo tuache chuki tujenge amani ya nchi yetu bila kufanya hivyo hatuwezi kupata maendeleo,”alisema Mangula na kuongeza kuwa;“Nashangaa na kushitushwa na viongozi wa dini wanapojiingiza na kubariki chuki, wanamkosea Mungu.
Machafuko yakishatokea hakuna atakayesalimika kwa kusema mimi ni kiongozi wa dini."Alieleza kuwa kazi ya serikali ni kuwajengea nyumba bali mazingira mazuri wananchi ili wajijenge na kujifanyia maendeleo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philipo Mangula akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM wa Mkoa wa Mara jana alipowasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi.Kushoto bi Mwenyekiti wa CCM mkoani Mara Samuel Kiboye Namba Tatu na wa pili kutoka kulia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ( NEC) Mkoa wa Mara Christopher Gachuma. Picha zote na Baltazar Mashaka.
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Mara, Samuel Kiboye Namba Tatu (kulia), akizungumza na baadhi ya viongozi na wana CCM waliojitokez kumpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philipo Mangula wa pili kutoka kushoto.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MANGULA AONYA VIONGOZI WA DINI, WANASIASA WANOVURUGA AMANI NCHINI
yaani makala yote MANGULA AONYA VIONGOZI WA DINI, WANASIASA WANOVURUGA AMANI NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MANGULA AONYA VIONGOZI WA DINI, WANASIASA WANOVURUGA AMANI NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/mangula-aonya-viongozi-wa-dini.html
0 Response to "MANGULA AONYA VIONGOZI WA DINI, WANASIASA WANOVURUGA AMANI NCHINI"
Post a Comment