Hajjat, Batuli Mziya hawataka WANAWAKE kushikamana

Hajjat, Batuli Mziya hawataka WANAWAKE kushikamana - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Hajjat, Batuli Mziya hawataka WANAWAKE kushikamana, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Hajjat, Batuli Mziya hawataka WANAWAKE kushikamana
kiungo : Hajjat, Batuli Mziya hawataka WANAWAKE kushikamana

soma pia


Hajjat, Batuli Mziya hawataka WANAWAKE kushikamana



Mh. Batuli Mziya akiwa na WANAWAKE wa Wilaya ya Kinondoni Kumwakilisha Mkuu wa Wilaya Ilala Sophia Mjema katika  Maulidi ya WANAWAKE wa Msasani Dar es Salaam jana.Katika Maulid hiyo Batuli alikutana na aliyekuwa kiongozi wa WANAWAKE wa Dini ya Kiislam Bi.Aisha Sululu.(Heri Shaban)

Na Heri Shaaban
Mwamba wa habari
 WANAWAKE nchini  wametakiwa kushikamana na kujenga umoja  katika kutafuta MAENDELEO .

Hayo yalisemwa na Mjumbe wa Kamati ya utekekezaji Umoja wa WANAWAKE( UWT) Wilaya ya Ilala Hajjat , Batuli Mziya katika Maulidi ya WANAWAKE wa Msasani Bonde  la Mpunga Wilayani Kinondoni ambapo Batuli alimwakilisha mkuu wa Wilaya Ilala Sophia Mjema.

Alisema MAENDELEO ya WANAWAKE uletwa na WANAWAKE wenyewe amewataka wajenge umoja na kushikamana katika kutafuta maendeleo na kukuza uchumi wa Tanzania ya Viwanda.

" Nawaomba wanawake wa Kinondoni wa Madrassa Til Munawwara na wanawake wengine kuungana na serikali yetu kumsaidia Rais kwani fursa zipo kwa wanawake za kuwezeshwa kiuchumi katika kukuza maendeleo" alisema Hajjat,  Batuli.

Hajjat, Batuli alisema WANAWAKE ndio wajenga nyumba na wabomoa nyumba katika familia mwanamke ndio mstari wa Mbele hivyo pia tunatakiwa kusimamia fursa zote za uchumi ambazo zinajitokeza kwa upande wa wanawake.

Akizungumzia dini amewataka WANAWAKE kujistili  maungo yao kwani dini zote zinazuia mwanamke kuacha maungo wazi.

Aliwapongeza WANAWAKE wa Kinondoni kwa kuandaa maulidi hiyo ambapo aliwasisitiza kupeleka watoto madrasa  kusoma.

Aidha Batuli alisema mwanamke bora ni yule atakaye funga Funga ya Ramadhani na kuheshimu ndoa yake  kesho atafunguliwa mlango wa pepo.


Kwa upande wa risala ya Madrasati Munawwara iliyosomwa na Mariam Abdulmaliki alisema Madras a hiyo ina wanafunzi 85 ilianzishwa mwaka  2002 awali ilikuwa na wanafunzi saba.


Mariamu alisema changamoto ya madrasa hiyo inalea watoto katika mazingira magumu hivyo wamemuomba Mgeni rasmi Batuli Mziya afikishe Salam kwa Mkuu wa Wilaya Ilala Sophia Mjema  watatuliwe changamoto zao .

Alisema changamoto nyingine kuwalea Wanawake Wajane ambao hawana wanaume na wanawake ambao hawana uwezo.

" Sisi WANAWAKE wa Kinondoni Msasani tunakuomba mama Sophia Mjema utusaidie mikopo ya vikundi ambayo itatukomboa au MRADI wowote  utusaidie na Yatima na Wajane tuliokuwa nao" alisema Mariamu.



Hivyo makala Hajjat, Batuli Mziya hawataka WANAWAKE kushikamana

yaani makala yote Hajjat, Batuli Mziya hawataka WANAWAKE kushikamana Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Hajjat, Batuli Mziya hawataka WANAWAKE kushikamana mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/hajjat-batuli-mziya-hawataka-wanawake.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Hajjat, Batuli Mziya hawataka WANAWAKE kushikamana"

Post a Comment