title : ECO Bank Tanzania kufadhili wanafunzi shule za serikali
kiungo : ECO Bank Tanzania kufadhili wanafunzi shule za serikali
ECO Bank Tanzania kufadhili wanafunzi shule za serikali
Benki ya Eco nchini Tanzania kuanzia mwaka huu inaanzisha mpango wa kutoa zawadi ya ufadhili kwa wasichana wanaofanya vyema katika masomo yao kwenye shule za serikali.
Aidha pamoja na ufadhili huo ili kuwaweka katika hali ya kuwa na uzoefu na kazi zao wanazosomea, watakuwa wanahakikisha wakati wa likizo wanawafanyia mpango wa kujishughulisha na kazi hizo ili kuwa na uzoefu.
Hayo yamesema na Mkurugenzi Mkuu benki hiyo nchini Mwanahiba Mzee wakati wa hafla ya mchapalo iliyofanyika hoteli ya Serena kusherehekea mafanikio ya mwanamke katika Siku ya Wanawake duniani mwishoni mwa wiki.
Alisema taasisi yake inaona umuhimu wa kumwezesha mtoto wa kike kusonga mbele kama moto wa taasisi hiyo ya kifedha unavyosema ‘press for progress’ ikimaananisha kujikita katika kutafuta maendeleo.
Alisema mwanamke anafanyakazi nyingi hivyo ni vyema kumwandaa tangu mapema ili kujua majukumu yake kama mzalishaji mkuu kwenye familia.
Alisema kwa sasa hawajaamua wanaanzia ngazi gani za ufadhili, lakini wanataka kufanya kitu tofauti chenye kulenga kupromoti maendeleo ya mtoto wa kike kama maazimio ya Beijing yanavyotaka kufikia asilimia hamsini kwa hamsini katika ngazi za kiutendaji.
Mkurugenzi Mkuu Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee akizungumza kabla ya mgeni rasmi ambapo alielezea kwa undani safari ya maisha kama mwanamke wakati hafla mchapalo ya kusherehekea mafanikio ya mwanamke katika Siku ya Wanawake duniani iliyoandaliwa na Eco Bank Tanzania na kufanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mgeni rasmi Mwanasiasa Mkongwe nchini na mpigania haki za wanawake, Mama Getrude Mongella akitoa nasaha zake kwa wageni waalikwa na wafanyakazi wa Eco Bank Tanzania (hawapo pichani) wakati wa hafla mchapalo ya kusherehekea mafanikio ya mwanamke katika Siku ya Wanawake duniani iliyoandaliwa na Eco Bank Tanzania na kufanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Vodacom Tanzania, Nandi Mwiyombela akijitambulisha na ku-‘share’ uzoefu sambamba na kubadilishana mawazo wakati wa hafla mchapalo ya kusherehekea mafanikio ya mwanamke katika Siku ya Wanawake duniani iliyoandaliwa na Eco Bank Tanzania na kufanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mkuu Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee akimpongeza Mgeni rasmi Mwanasiasa Mkongwe nchini na mpigania haki za wanawake, Mama Getrude Mongella kwa nasaha nzuri alizotoa wakati wa hafla mchapalo ya kusherehekea mafanikio ya mwanamke katika Siku ya Wanawake duniani iliyoandaliwa na Eco Bank Tanzania na kufanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano Ecobank Tanzania, Furaha Samalu
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano Ecobank Tanzania, Furaha Samalu (katikati), Meneja wa Mawasilisho ya Fedha Eco Bank Tanzania, Samiha Abdul (kulia) katika picha ya pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Vodacom Tanzania, Nandi Mwiyombela wakati wa hafla mchapalo ya kusherehekea mafanikio ya mwanamke katika Siku ya Wanawake duniani iliyoandaliwa na Eco Bank Tanzania na kufanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mmiliki wa Jarida la Bang Magazine, Emelda Mwamanga (kushoto) na Mtangazaji wa kipindi cha Luninga cha Jikoni na Marion kinachorushwa na DStv, Marion Elias (kulia) wakisikiliza kwa umakini shuhuda mbalimbali za wanawake waliopigia hatua kiuchumi katika ujasiriamali wakati wa hafla mchapalo ya kusherehekea mafanikio ya mwanamke katika Siku ya Wanawake duniani iliyoandaliwa na Eco Bank Tanzania na kufanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia mada wakati wa hafla mchapalo ya kusherehekea mafanikio ya mwanamke katika Siku ya Wanawake duniani iliyoandaliwa na Eco Bank Tanzania na kufanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala ECO Bank Tanzania kufadhili wanafunzi shule za serikali
yaani makala yote ECO Bank Tanzania kufadhili wanafunzi shule za serikali Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ECO Bank Tanzania kufadhili wanafunzi shule za serikali mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/eco-bank-tanzania-kufadhili-wanafunzi.html
0 Response to "ECO Bank Tanzania kufadhili wanafunzi shule za serikali"
Post a Comment