title : WANANCHI WA MKAMBA WAISHUKURU SERIKALI.
kiungo : WANANCHI WA MKAMBA WAISHUKURU SERIKALI.
WANANCHI WA MKAMBA WAISHUKURU SERIKALI.
Mwambawahabari

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mkamba wilayani mkuranga
Wananchi wa kata ya Mkamba wilayani Mkuranga wameishukuru serikali kuwa kuwapatia fedha za kuboresha kituo chao cha afya.
Shukrani hizo zimetolewa na wananchi hao wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo alipotembelea kijijini hapo.
Akizungumza na wananchi wa kata ya Mkamba Waziri Jafo amewapongeza wananchi hao kwa kuanza maandalizi ya ujenzi wa miundombinu itakayojengwa na fedha hizo zilizo tolewa na serikali.
Jafo amempongeza mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Abdullahi Ulega kwa kupeleka kilio cha wananchi wa Mkamba hadi serikali kufanya maamuzi ya kupeleka milioni 400 za ujenzi wa miundombinu na milioni 300 zingine zimepelekwa MSD kwaajili ya ununuzi wa vifaa.
Aidha, Jafo amewaagiza viongozi wa Mkuranga kwenda kujifunza katika kituo cha afya Maneromango kilichopo wilayani Kisarawe ili waone jinsi matumizi ya force account yalivyoleta manufaa katika ujenzi wa vituo vya afya hapa nchini.
Baada ya kikao na wananchi wa Mkamba Waziri Jafo alifanya ukaguzi wa barabara inayounganisha wilaya ya Mkuranga na wilaya ya Kisarawe kupitia bonde la Mkuruili na amewaagiza mameneja wa TARURA wa wilaya ya Mkuranga na wilaya ya Kisarawe kukaa pamoja kuiwekea mikakati barabara hiyo ili wananchi wa maeneo hayo waweze kuunganishwa vyema.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na baadhi ya viongozi walio shiriki ukaguzi wa barabara ya mkamba kwenda Msanga ambayo inahitaji matengenezo makubwa
Hivyo makala WANANCHI WA MKAMBA WAISHUKURU SERIKALI.
yaani makala yote WANANCHI WA MKAMBA WAISHUKURU SERIKALI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANANCHI WA MKAMBA WAISHUKURU SERIKALI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/wananchi-wa-mkamba-waishukuru-serikali.html
0 Response to "WANANCHI WA MKAMBA WAISHUKURU SERIKALI."
Post a Comment