title : VIJANA WA MOROGORO WANUFAIKA NA AJIRA UJENZI RELI MWENDO KASI ‘SGR’
kiungo : VIJANA WA MOROGORO WANUFAIKA NA AJIRA UJENZI RELI MWENDO KASI ‘SGR’
VIJANA WA MOROGORO WANUFAIKA NA AJIRA UJENZI RELI MWENDO KASI ‘SGR’
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe ( wa kwanza kulia) asikiliza maelezo ya mtaalamu wa Kampuni ya Uhandisi ya MotaEngil Afrika - Tanzania ya ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge) eneo la Ngerengere kutoka kwa Mpima ardhi wa Kampuni hiyo , Juma Sospeter , wakati wa ziara yake na wajumbe wa kamati ya ulinzi na salama ya mkoa na wilaya ya Morogoro alipotembelea eneo la ujenzi wa kambi ya kampuni hiyo na njia ya reli ya kisasa ya “SGR “ katika kata ya Ngerengere , wilayani humo.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe ( wa pili kulia) asikiliza maelezo ya mtaalamu wa Kampuni ya Uhandisi ya MotaEngil Afrika - Tanzania ya ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge) ambaye ni Mpima ardhi , Juma Sospeter , wakati wa ziara yake na wajumbe wa kamati ya ulinzi na salama ya mkoa na wilaya ya Morogoro alipotembelea eneo la ujenzi wa kambi ya kampuni hiyo na njia ya reli ya kisasa ya “SGR “ eneo la kata ya Ngerengere , na ( kutoka kushoto) ni mkuu wa wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo akizungumza jambo na Mhandisi mwendeshaji wa kampuni hiyo , Filipe Ataide. ( Picha na John Nditi).
Baadhi ya wataalamu wa Kitanzania wa Kampuni ya Uhandisi ya MotaEngil Afrika - Tanzania ya ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge) wakiendelea na kazi zao za hatua ya awali ya ujenzi huo eneo la Ngerengere wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe na wajumbe wa kamati ya ulinzi na salama ya mkoa na wilaya ya Morogoro walipotembelea eneo la ujenzi wa kambi ya kampuni hiyo na njia ya reli ya kisasa , “SGR “ katika kata ya Ngerengere , wilayani humo.
Na John Nditi, Morogoro
MKUU wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe ameitaka Kampuni ya Uhandisi ya MotaEngil Afrika - Tanzania ya ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge) kuhakikisha inawatumia wafanyakazi wa kitanzania waliopo katika maeneo ya ujenzi wa mradi kwenye ajira zisizo hitaji utaalamu zaidi. Dk Kebwe alisema hayo alipokuwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na wilaya ya Morogoro wakati alipotembelea eneo la ujenzi wa kambi ya kampuni hiyo na njia ya reli ya kisasa inayotarajiwa kujengwa ,kata ya Ngerengere , wilayani humo.
Mkuu huyo wa mkoa alisema , suala la ajira katika miradi kama hiyo mara nyingi limeleta tatizo kubwa , lakini kutokana na maelezo ya uongozi wa Kampuni pamoja na wa Serikali za kijiji na Kata ya Ngerengere kuwa upo utaratibu mzuri wa kushirikisha viongozi hao kuwapata wafanyakazi kwenye kazi zisizo na utaalamu.
“ Hatuja pata matatizo na wanaendelea vyema na kukamilishaji wa ujenzi wa kambi na kuanza njia ya reli ya SGR “ alisema Dk Kebwe .
Pamoja na hayo aliitaka Kampuni hiyo kuweka kipaumbele cha ajira kwa wakazi wa maeneo ya mradi na si kuchukua watu wa mbali , na kwamba kutokana na utaratibu uliowekwa kwa kushirikisha viongozi wa serikali za vijiji na kata utaondoa malalamiko na hiyo ni miongoni mwa sera ya kampuni. Mkuu huyo wa mkoa , aliitaka kampuni hiyo kutekeleza majukumu yake ya ujenzi wa reli ya kisasa kama mkataba ulivyo na kwa kuzingatia kauli ya Rais Dk John Magufuli wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa mradi huo ya kuwapata kukamil;ishaji uwe ndani ya miezi 24.
Pia aliwataka viongozi wa vijiji na kata vilivyopo jirani na eneo hilo kushirikiana na wananchi ili kuhakikisha mradi huo unalindwa kwa lengo la kumwezesha mkandarasi kumaliza kwa wakati.
“ Wale wezi wa mafuta , vipiri na vitu vingine vya mradi huu washughulikiwe kikamilifu wanaponainika “ aliangiza Dk Kebwe kwa viongozi wa Serikali za vijiji vya kata ya Ngerengere.
Kwa upande wao ,Mpima ardhi wa Kampuni hiyo , Juma Sospeter pamoja na msimamizi wa maeneo ya ujenzi wa kambi hiyo Erick Mtasiwa ka nyakati tofauti wakitoa maelezo kwa niaba ya kampuni, walisema zaidi ya vijana 50 kutoka vijiji vya tarafa ya Ngerengere, wamenufaika na ajira za mkataba za kufanya kazi mbaimbali. Walisema , kampuni imezingatia maelekezo na miongozo inayotolewa na serikali kuyataka makampuni yanayo fanyashughuli mbalimbali ikiwemo ujenzi kuhakikisha inawatumia wafanyakazi wa kitanzania hususani katika ajira zisizo hitaji utaalam zaidi.
Awali, Mhandisi mwendeshaji wa kampuni ya MotaEngil Afrika - Tanzania , Filipe Ataide alisema mpaka sasa hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza na wamepenga kukamilisha mradi huo kuzingatia makubaliano yaliyomo ndani ya mkataba na kwa ushauri wa Rais. Ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge) kwa awamu kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro inatarajiwa kukamilika Oktoba 2019, ikiwa na urefu wa kilometa 300 na steshani sita na inajengwa na Kampuni ya Uhansisi ya Mota-Engil Afrika – Tanzania.
Hivyo makala VIJANA WA MOROGORO WANUFAIKA NA AJIRA UJENZI RELI MWENDO KASI ‘SGR’
yaani makala yote VIJANA WA MOROGORO WANUFAIKA NA AJIRA UJENZI RELI MWENDO KASI ‘SGR’ Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VIJANA WA MOROGORO WANUFAIKA NA AJIRA UJENZI RELI MWENDO KASI ‘SGR’ mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/vijana-wa-morogoro-wanufaika-na-ajira.html
0 Response to "VIJANA WA MOROGORO WANUFAIKA NA AJIRA UJENZI RELI MWENDO KASI ‘SGR’"
Post a Comment