WAZIRI MKUU AKUTANA NA NAIBU SPIKA WA BUNGE LA CAMEROON NA MWENYEKITI WA KAMATI TENDAJI YA CPA

WAZIRI MKUU AKUTANA NA NAIBU SPIKA WA BUNGE LA CAMEROON NA MWENYEKITI WA KAMATI TENDAJI YA CPA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MKUU AKUTANA NA NAIBU SPIKA WA BUNGE LA CAMEROON NA MWENYEKITI WA KAMATI TENDAJI YA CPA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MKUU AKUTANA NA NAIBU SPIKA WA BUNGE LA CAMEROON NA MWENYEKITI WA KAMATI TENDAJI YA CPA
kiungo : WAZIRI MKUU AKUTANA NA NAIBU SPIKA WA BUNGE LA CAMEROON NA MWENYEKITI WA KAMATI TENDAJI YA CPA

soma pia


WAZIRI MKUU AKUTANA NA NAIBU SPIKA WA BUNGE LA CAMEROON NA MWENYEKITI WA KAMATI TENDAJI YA CPA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea taarifa ya utendaji ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kimataifa (CPA - INERNTIONAL) ya mwaka 2018 kutoka kwa Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA,  Emilia Monjowa Lifaka, baada ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma Aprili 4, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kimatifa (CPA-INTERNATIONAL), Emilia Monjowa Lifaka, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dodoma, Aprili 4, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kimatifa (CPA-INTERNATIONAL), Emilia Monjowa Lifaka (wa pili kushoto) baada ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dodoma, Aprili 4, 2019. Wa tatu kulia ni Mbunge wa Babati Vijijni, Vrajilal Jitu Son na wa pili kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum na Mwakilishi wa CPA tawi la Tanzania, Maria Kangoye.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimwonyesha mandhari ya jiji la Dodoma, Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kimatifa (CPA-INTERNATIONAL), Emilia Monjowa Lifaka baada ya mazungumzo yao ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dodoma, Aprili 4, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).




SERIKALI ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA CPA-MAJALIWA


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali itatoa ushirikiano kwa Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA – Africa)

wanaotarajia kufanya mkutano wao Novemba 2019, nchini Tanzania.

Ametoa kauli hiyo jana (Alhamisi, Aprili 4, 2019) alipokutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Chama cha Mabunge ya Madola Kanda ya Afrika, Mheshimiwa Emilia Monjolwa Lifaka.

Waziri Mkuu alisema Bunge na Serikali nchini wanafanya kazi kwa kushirikiana, hivyo amemuhakikishia Mhe. Emilia ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Cameroon kuwa Serikali itatoa ushirikiano unaohitajika kwa CPA ili kufanikisha malengo tarajiwa

Pia, Waziri Mkuu alisema Serikali inaushukuru uongozi wa CPA kwa kutoa ushirikiano stahiki kwa wabunge wa Bunge la Tanzania ambao ni wanachama wa CPA 

Kwa upande wake, Mhe. Emilia aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuzingatia usawa wa kijinsia na kutoa fursa kwa wanawake katika nafasi za uongozi ikiwa ni pamoja na idadi kubwa ya wabunge wanawake kufikia asilimia zaidi ya 30 ya wabunge wote.

Kadhalika, Mwenyekiti huyo alisema Maspika wa CPA – Afrikawanaotarajia kufanya mkutano Novemba 2019, katika jiji la Arusha nchini Tanzania wameridhika sana kwa ahadi ya Serikali ya Tanzania kuhusu ushirikiano na maandalizi mazuri.

Mkutano huo wa Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika utajadili ajenda mbalimbali pamoja na kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya nchi hizo kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo.


Hivyo makala WAZIRI MKUU AKUTANA NA NAIBU SPIKA WA BUNGE LA CAMEROON NA MWENYEKITI WA KAMATI TENDAJI YA CPA

yaani makala yote WAZIRI MKUU AKUTANA NA NAIBU SPIKA WA BUNGE LA CAMEROON NA MWENYEKITI WA KAMATI TENDAJI YA CPA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU AKUTANA NA NAIBU SPIKA WA BUNGE LA CAMEROON NA MWENYEKITI WA KAMATI TENDAJI YA CPA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/04/waziri-mkuu-akutana-na-naibu-spika-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI MKUU AKUTANA NA NAIBU SPIKA WA BUNGE LA CAMEROON NA MWENYEKITI WA KAMATI TENDAJI YA CPA"

Post a Comment