title : UPELELEZI KESI YA UTAKATISHAJI FEDHA DOLA 150,000 BADO HAUJAKAMILIKA
kiungo : UPELELEZI KESI YA UTAKATISHAJI FEDHA DOLA 150,000 BADO HAUJAKAMILIKA
UPELELEZI KESI YA UTAKATISHAJI FEDHA DOLA 150,000 BADO HAUJAKAMILIKA
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, upelelezi wa kesi ya utakatishaji fedha kiasi cha Dola za Marekani 150,000 inayomkabili Mhasibu wa Ubalozi wa Tanzania Maputo nchini Msumbiji, Joyce Moshi (56) bado haujakamilika.
Mshtakiwa Moshi anayeishi Temeke anakabiliwa na mashtaka tisa yakiwamo ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi, wizi akiwa mtumishi wa umma na utakatishaji wa fedha.
Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa kesi hiyo leo imekuja kwa kutajwa kwani upelelezi bado haujakamilika na wanasubiri nyaraka kutoka Msumbiji ili kukamilisha upelelezi. Hakimu Shaidi ameutaka upande wa mashtaka kuendelea kufuatilia hizo nyaraka ili upelelezi ukamilike na kesi imeahirishwa hadi Machi 13, mwaka 2018.
Mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa Oktoba 25, mwaka 2016 katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo Maputo nchini Msumbiji alighushi barua ya Oktoba 25, mwaka 2016.
Akijaribu kuonesha kuwa ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji imeilekeza Benki ya Millennium BIM ya Maputo, kuhamisha dola za Marekani 10,000 kutoka kwenye akaunti namba 79667362 kwenda akaunti namba 182283177 inayomilikiwa na Mushi na akaunti hizo zote zipo kwenye benki hiyo iliyopo katika tawi la Julius Nyerere Maputo, wakati akijua si kweli.
Anadaiwa kuwa Februari 10, mwaka 2017 katika ofisi za Ubalozi Maputo Msumbiji, alighushi barua akionyesha kuwa ubalozi huo umeielekeza Benki ya Millennium BIM ya Maputo, kuhamisha dola za Marekani 10,000 kutoka akaunti namba 79667362 kwenda akaunti namba 182283177 inayomilikiwa na Moshi.
Aprili 12, mwaka 2017 katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Maputo nchini Msumbiji, mshtakiwa huyo anadaiwa alighushi barua ya Aprili 12, mwaka 2017 akijaribu kuonesha kuwa ubalozi huo umeielekeza Benki ya Millennium BIM ya Maputo, kuhamisha dola za Marekani 40,000 kutoka akaunti namba 79667362 kwenda akaunti namba 182283177.
Oktoba 25, mwaka 2016 katika Benki ya Millennium BIM iliyopo tawi la Julius Nyerere Maputo nchini Msumbiji, aliwasilisha kwenye benki hiyo nyaraka za kughushi ambayo ni barua ya Oktoba 25, 2016 akionesha kuwa Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji umeelekeza benki hiyo kuhamisha dola za Marekani 10,000 kutoka kwenye akaunti ya benki hiyo kwenda kwenye akaunti inayomilikiwa na mshitakiwa huyo.
Iliendelea kudai kuwa Februari 10, 2017 katika benki hiyo, Moshi alitoa nyaraka za uongo kuonesha kwamba Ubalozi umeelekeza kuhamisha dola za Marekani 10,000 kwenda kwenye akaunti ya Moshi.
Aprili 12, 2017 katika maeneo ya benki hiyo mshtakiwa huyo aliwasilisha barua ya Aprili 12, 2017 kuonesha kuwa ubalozi umeelekeza kuamisha dola za Marekani 40,000 kwenda kwenye akaunti ya Moshi.
Katika tarehe tofauti kati ya Oktoba 25,mwaka 2016 na Aprili 12, mwaka 2017 akiwa mtumishi wa umma kama Mhasibu wa Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji, aliiba dola za Marekani 150,000 mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Inadaiwa kati ya Oktoba 25, 2016 na Aprili 12, 2017 katika ofisi za ubalozi huo, Moshi alijipatia dola za Marekani 150,000.
Mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa, kati ya Oktoba 25, 2016 na Aprili 12, 2017 katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania uliopo Maputo nchini Msumbiji na Benki ya Millenium BIM tawi la Julius Nyerere Maputo, alijipatia dola za Marekani 150,000 wakati akijua fedha hizo ni zao la kughushi.
Hivyo makala UPELELEZI KESI YA UTAKATISHAJI FEDHA DOLA 150,000 BADO HAUJAKAMILIKA
yaani makala yote UPELELEZI KESI YA UTAKATISHAJI FEDHA DOLA 150,000 BADO HAUJAKAMILIKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UPELELEZI KESI YA UTAKATISHAJI FEDHA DOLA 150,000 BADO HAUJAKAMILIKA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/upelelezi-kesi-ya-utakatishaji-fedha.html
0 Response to "UPELELEZI KESI YA UTAKATISHAJI FEDHA DOLA 150,000 BADO HAUJAKAMILIKA"
Post a Comment