UHAMIAJI YAWACHUNGUZA WATOTO WATATU RAIA WA RWANDA KWA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI

UHAMIAJI YAWACHUNGUZA WATOTO WATATU RAIA WA RWANDA KWA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UHAMIAJI YAWACHUNGUZA WATOTO WATATU RAIA WA RWANDA KWA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UHAMIAJI YAWACHUNGUZA WATOTO WATATU RAIA WA RWANDA KWA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI
kiungo : UHAMIAJI YAWACHUNGUZA WATOTO WATATU RAIA WA RWANDA KWA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI

soma pia


UHAMIAJI YAWACHUNGUZA WATOTO WATATU RAIA WA RWANDA KWA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI

Na Jumbe Ismailly, Singida
IDARA ya Uhamiaji Mkoa wa Singida inawashikilia kwa uchunguzi watoto wa kike watatu raia wa  Rwanda wenye umri chini ya miaka 18 kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria.

Kaimu Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Singida,Kamishna Msaidizi, Angela Shija amesema watoto hao wenye umri kati ya miaka 9 na 13 walikamatwa Januanri 30,mwaka 2018 wilayani Manyoni.

Amesema walikuwa  wakitokea nchini Rwanda wakielekea nchini Zambia kuwaona wazazi wao.

“Januari 30 mwaka 2018,  ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Singida ilifanikiwa kuwakamata watoto wa kike watatu raia wa Rwanda.

"Walikamatwa wilayani Manyoni mkoani Singida wakiwa kwenye basi namba T 265 BFY mali ya Kampuni ya Katagi,” amefafanua Kamishina huyo msaidizi

Kwa mujibu wa Ofisa Uhamiaji  Idara ya Uhamiaji ilifanikiwa kuwakamata watoto hao kutokana na taarifa za raia wema na watoto hao wamedai wanaelekea nchini Zambia kuwaona wazazi wao.

Hata hivyo Kamishina Msaidizi huyo wa Jeshi la Uhamiaji limeweka bayana kuwa Idara ya Uhamiaji mkoani Singida inaendelea na uchunguzi ili kubaini watu waliojihusisha na biashara hiyo ya   usafirishaji wahamiaji haramu.

Aidha Kaimu Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Singida ametoa mwito kwa wananchi  kujenga utamaduni wa kutoa taarifa kwenye ofisi zao au kwenye vituo vya polisi vilivyo karibu mara wanapowaona watu wasiowafahamu.

Amefafanua kuwa taarifa hizo zitaisaisi Uhamiaji kufanyia kazi za kubaini matukio ya watu wa aina hiyo na kuwachukulia hatua za kisheria.

Amesisitiza baada ya uchunguzi kukamilika na kuwabaini waliohusika katika biashara hiyo ya kuwasafirisha,na kwa sababu wana umri chini ya miaka 18,watoto hao watarudishwa nyumbani kwa wazazi wao nchini Rwanda.
 Watoto wa kike watatu raia wa Rwanda wenye umri chini ya miaka 18 kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria wakiwa kwenye ofisi za idara hiyo Mkoa Singida
 Baadhi ya Maafisa Uhamiaji waliopo katika Ofisi za Mkoa wa Singida (Picha zote Na Jumbe Ismailly)


Hivyo makala UHAMIAJI YAWACHUNGUZA WATOTO WATATU RAIA WA RWANDA KWA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI

yaani makala yote UHAMIAJI YAWACHUNGUZA WATOTO WATATU RAIA WA RWANDA KWA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UHAMIAJI YAWACHUNGUZA WATOTO WATATU RAIA WA RWANDA KWA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/uhamiaji-yawachunguza-watoto-watatu.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "UHAMIAJI YAWACHUNGUZA WATOTO WATATU RAIA WA RWANDA KWA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI"

Post a Comment