TEA YAKABIDHI MRADI UKARABATI SHULE YA WASICHANA KONDOA

TEA YAKABIDHI MRADI UKARABATI SHULE YA WASICHANA KONDOA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TEA YAKABIDHI MRADI UKARABATI SHULE YA WASICHANA KONDOA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TEA YAKABIDHI MRADI UKARABATI SHULE YA WASICHANA KONDOA
kiungo : TEA YAKABIDHI MRADI UKARABATI SHULE YA WASICHANA KONDOA

soma pia


TEA YAKABIDHI MRADI UKARABATI SHULE YA WASICHANA KONDOA

Na: Sekela Mwasubila - Kondoa

Mamlaka ya Elimu Tanzania imekabidhi rasmi mradi wa ukarabati wa Shule ya Wasichana Kondoa tukio lililofanyika katika ukumbi wa shule hiyo hivi karibuni.

Akikabidhi mradi huo Kaimu Mkurugenzi wa Mmlaka ya Elimu Tanzania Graceana Shirima alisema ni matumaini yao kuwa fedha hizo zitatumika kwa ufanisi mkubwa na makusudio waliyoyaweka na matokeo yake yaonekae kwani iliyotolewa ni nyingi.

Aidha aliongeza kuwa lengo la ukarabati huo ni kuhakikisha kuwa shule inakuwa na mazingira mazuri kwa ajili ya kupata elimu iliyokusudiwa na kuongeza ufaulu kwani miundombinu ya maabara, maktaba na madarasa vyote vitakarabatiwa na kuwa na mwonekano mzuri kwa mwanafunzi kusoma.

“Tuna imani uongozi wa Halmashauri ya Mji na Bodi ya Shule hawatatuangusha katika usimamizi na watatumia fedha hizi kwa umakini mkubwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha taratibu zote za manunuzi zinazingatiwa na hatutasita kumchukulia hatua mtu yoyote atakayekwenda kinyume na taratibu za manunuzi sababu mradi huu force akaunti ambayo inatumia jamii zaidi” Alisema Bi Graceana

Akiongea kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mh. Hamza Mafita alisema wanaishukuru serikali kwa kuwaletea fedha zote za mradi kwani fedha hizo zitabakia kwa wananchi wa Kondoa kwani mafundi watanunua vifaa vyote Kondoa na mafundi ni wenyeji wa Kondoa na kuwataka mafundi kumaliza mradi huo kwa wakati na haoni sababu ya kuchelewa ikiwa fedha zote zipo.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Khalifa Kondo akipokea mradi huo alisema kuwa anashukuru kupata mradi huo sababu ingekuwa ni jukumu la Halmashauri kukarabati kwa kutumia mapato ya ndani na kuahidi kuzisimamia fedha hizo kwa kushirikiana na wataalam wa Halmashauri na Bodi ya shule ili kuhakikisha lengo la mradi linakamilika.

Mamlaka ya Elimu Tanzania imetoa kiasi zaidi ya bilioni kumi kwa ajili ya ukarabati wa shule kongwe Tanzania ikiwemo Shule ya Wasichana Kondoa ambapo imepewa shilingi bilioni moja kwa ajili ya ukarabati wa majengo ya shule hiyo.
Sehemu ya Mabweni yanayoendelea na ukarabati katika shule ya Wasichana Kondoa
Kaimu Mkurugenzi wa Malmaka ya Elimu Tanzania Bi Graceana Shirima (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Mji Kondoa Khalifa Kondo orodha ya vifaa kwa ajili ya ukarabati wa Shule ya Wasichana Kondoa. 
Mafundi wakiendelea na uchimbaji wa shimo la maji machafu ikiwa ni sehemu ya ukarabati wa mfumo wa miundombinu ya maji machafu katika shule ya wasichana Kondoa
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi Graceana Shirima akiwa katika picha ya pamoja na Walimu wa Shule ya Wasichana Kondoa.
Picha ya Uongozi wa Mamlaka ya Elimu na Halmashauri ya Mji katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Wasichana Kondoa.



Hivyo makala TEA YAKABIDHI MRADI UKARABATI SHULE YA WASICHANA KONDOA

yaani makala yote TEA YAKABIDHI MRADI UKARABATI SHULE YA WASICHANA KONDOA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TEA YAKABIDHI MRADI UKARABATI SHULE YA WASICHANA KONDOA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/tea-yakabidhi-mradi-ukarabati-shule-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TEA YAKABIDHI MRADI UKARABATI SHULE YA WASICHANA KONDOA"

Post a Comment