title : Wafanyakazi HESLB waaswa kuwa wabunifu
kiungo : Wafanyakazi HESLB waaswa kuwa wabunifu
Wafanyakazi HESLB waaswa kuwa wabunifu
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe amewataka wafanyakazi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kuongeza ubunifu ili kuondokana na changamoto wanazokutana nazo.
Prof. Mdoe amesema hayo leo (Jumatatu, Novemba 13, 2017) alipokua akiongea na Menejimenti ya HESLB katika ziara aliyoifanya katika makao makuu ya HESLB jijini Dar es Salaam.
“Pamoja na mafanikio mnayoyapata hasa katika ukusanyaji wa mikopo lakini bado kuna changamoto…zikiwemo za malalamiko ya vigezo vya utoaji mikopo ambavyo mnahitaji kuwa wabunifu kwa kuwashirikisha wadau,” amesema kiongozi huyo katika ziara yake ya kikazi.
Kwa mujibu wa Prof. Mdoe, nia ya Serikali ni kuona malalamiko yote ya wadau yanatafutiwa ufumbuzi kwa haraka, na ili hilo litimizwe ni muhimu kwa wafayakazi wa taasisi za umma kuwa wabunifu zaidi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe akiongea na menejimenti ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wakati wa ziara yake ya kikazi katika Ofisi za HESLB jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Nov 13, 2017). Keshoto ni Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka Wizara ya Elimu Prof. Sylvia Temu na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru. (Picha na HESLB)
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe (katikati) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru wakati wa ziara yake ya kikazi katika Ofisi za HESLB jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Nov 13, 2017). Keshoto ni Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka Wizara ya Elimu Prof. Sylvia Temu. (Picha na HESLB)
Baadhi ya wajumbe wa menejimenti ya Bodi ya Mikopo katika mkutano na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe ambaye amefanya ziara yake ya kikazi katika Ofisi za HESLB jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Nov 13, 2017). (Picha na HESLB) .
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Wafanyakazi HESLB waaswa kuwa wabunifu
yaani makala yote Wafanyakazi HESLB waaswa kuwa wabunifu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wafanyakazi HESLB waaswa kuwa wabunifu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/wafanyakazi-heslb-waaswa-kuwa-wabunifu.html
0 Response to "Wafanyakazi HESLB waaswa kuwa wabunifu"
Post a Comment