title : TAA YAPEWA WIKI 2 KUKUSANYA MADENI YOTE
kiungo : TAA YAPEWA WIKI 2 KUKUSANYA MADENI YOTE
TAA YAPEWA WIKI 2 KUKUSANYA MADENI YOTE
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akisisitiza
jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu mipango ya
Serikali ya kuendeleza kiwanja cha Ndege Mwanza kwa kuiboresha
miundombinu ili kiwanja hicho kiwe cha Kimataifa, wakati alipokagua
maendeleo ya upanuzi wa kiwanja hicho.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametoa wiki
mbili kwa Mamlaka ya Viwanja Ndege Nchini (TAA), kukusanya fedha za
madeni ambayo inadai kutoka kwa watoa huduma mbalimbali katika viwanja
vyote vya ndege ili ziweze kutumika kuendeleza miundombinu.
Kauli
hiyo ametoa jijini Mwanza, baada kukagua maendeleo ya upanuzi wa
kiwanja cha ndege na hali ya uendeshaji katika kiwanja hicho ambapo
amebaini kuwa kuna madeni ambayo yanaweza kulipika na kuweza kurahisisha
shughuli za kiuendeshaji ikiwemo kujenga uzio ili kuongeza usalama
kiwanjani hapo.
"Nataka TAA mkusanye madeni yote mnayodai, fedha
hizi zikipatikana zinaweza kutumika kujenga uzio kwa ajili ya kulinda
usalama wa uwanja ili wananchi wasiweze kuvamia na pia usalama wa ndege
zinazoruka na kutua", amesisitiza Prof. Mbarawa.
Amefafanua
kuwa kama Taasisi hizi zikikusanya madeni na watoa huduma wakalipa kodi
kwa wakati kutasaida Serikali kuboresha maendeleo ya miundombinu.
Kuhusu
maendeleo ya upanuzi wa kiwanja hicho. Prof. Mbarawa amesema
ameridhishwa na kasi ya ujenzi ambapo kwa sasa umefikia asilimia 60.
Ameongeza kuwa ujenzi huo unategemewa kumalizika mwezi Julai mwaka huu na utagharimu kiasi cha shilingi takribani bilioni 94.
Aidha amesema Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la abiria mara miradi inayoendelea kukamilika.
Naye
Msimamizi wa Kiwanja hicho ambaye ni Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara
(TANROADS), mkoa wa Mwanza, Mhandisi Joseph Mwami, amesema kazi
zinazoendelea kwa sasa ni pamoja na ujenzi wa jengo la kuongoza ndege,
eneo la maegesho na njia za kuruka na kutua ndege
Mhandisi
Mwami, amefafanua kuwa njia ya kuruka na kutua ndege katika kiwanja
hicho imeongezwa urefu wa mita 500 ili kuifanya kufikia urefu wa KM 3.5
ili kuwezesha ndege kubwa za kimataifa kuweza kutua na kuruka katika
kiwanja hicho.
Hivyo makala TAA YAPEWA WIKI 2 KUKUSANYA MADENI YOTE
yaani makala yote TAA YAPEWA WIKI 2 KUKUSANYA MADENI YOTE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAA YAPEWA WIKI 2 KUKUSANYA MADENI YOTE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/taa-yapewa-wiki-2-kukusanya-madeni-yote.html
0 Response to "TAA YAPEWA WIKI 2 KUKUSANYA MADENI YOTE"
Post a Comment