title : Shilingi milioni 208 zanufaisha kaya maskini TASAF Kishapu
kiungo : Shilingi milioni 208 zanufaisha kaya maskini TASAF Kishapu
Shilingi milioni 208 zanufaisha kaya maskini TASAF Kishapu
Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi.
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) imetoa sh. milioni 208.5 kwa ajili ya kuwezesha kaya maskini katika kipindi cha Januari hadi Februari.
Mratibu wa TASAF wilaya hiyo, Sospeter Nyamuhanga amebainisha hayo jana ambapo amesema fedha hizo zimetolewa kwa ajili ya kaya 5959 katika vijiji 78 vilivyopo wilaya humo.Alisema kuwa zoezi hilo limeendelea kupata mafanikio kutokana na walengwa wengi kufanyia kazi elimu wanayopewa kuhusu matumizi sahihi ya fedha hizo wanazowezeshwa.
Nyamuhanga aliongeza kuwa kutokana na ufuatiliaji unaofanyika nyakati tofauti baadhi ya kaya zimeonesha mabadiliko kimaisha ambapo zimetumia fedha hizo kuboresha maisha yao kwa kufanya shughuli mbalimbali za kujipatia kipato.
Alifafanua kuwa katika kaya hizo imebainika kuwa wanufaikaji wameweza kununua mifugo ikiwemo mbuzi, kondoo na kuku huku wengine wakifanya biashara ndogondogo.Aidha, alisema baadhi ya walengwa tayari wamebadilisha aina za makazi yao kutoka nyumba za tembe na nyasi za awali na kuanza kujenga nyumba za kisasa za bati hali inayoleta matumaini katika miradi kama hii.
“Lengo la mpango wa TASAF siku zote ni kuziwezesha kaya maskini kujikwamua kiuchumi na ndiyo maana mara kwa mara katika mazoezi haya tunatoa elimu ili kuwaelekeza namna bora kutumia fedha wanazowezeshwa,” alisema.
Zoezi la uwezeshaji Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) likiendelea katika kijiji cha Mwigumbi kata ya Mondo ambapo mmoja wa walengwa akiwawezeshwa ruzuku.
Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Sospeter Nyamuhanga (wa pili kulia waliosimama) akipata maelezo kuhusu zoezi hilo alipofika kufanya ufuatiliaji kijiji cha Wela kata ya Uchunga.
Sehemu ya walengwa wa TASAF wakiwa katika zoezi la uwezeshaji kwenye kijiji cha Mwigumbi kata ya Mondo.
Hivyo makala Shilingi milioni 208 zanufaisha kaya maskini TASAF Kishapu
yaani makala yote Shilingi milioni 208 zanufaisha kaya maskini TASAF Kishapu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Shilingi milioni 208 zanufaisha kaya maskini TASAF Kishapu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/shilingi-milioni-208-zanufaisha-kaya.html
0 Response to "Shilingi milioni 208 zanufaisha kaya maskini TASAF Kishapu"
Post a Comment