title : MAKONDA ASISITIZA MAKAMPUNI YA UDALALI KUFUATASHERIA ,WANAO KAMATA BODA BODA KWA KUWA PIGA WAONYWA
kiungo : MAKONDA ASISITIZA MAKAMPUNI YA UDALALI KUFUATASHERIA ,WANAO KAMATA BODA BODA KWA KUWA PIGA WAONYWA
MAKONDA ASISITIZA MAKAMPUNI YA UDALALI KUFUATASHERIA ,WANAO KAMATA BODA BODA KWA KUWA PIGA WAONYWA
Mwamba wa habari
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe.Paul Makonda amezitaka kampuni zote za udalali kujisalili ili kutambulika kisheria na kuweza kufahamu uhalali wa kazi zao lengo likiwa ni kuepuka watu wajanja wanaowakandamiza wananchi bila kuwa na sababu ya msingi.
Rc Makonda ameyasema hayo leo Katika mkutano na Madalali hao na kusema ni muhimu sana kufanya kazi na mamlaka zilizopo ili waweze kufanya kazi salama na wanaohudumiwa pia waweze kuwa salma na kuweza kuondokana na wale wanaovunja sheria na kuwakandamiza wananchi wanyonge wanaotafta haki zao.
"Nawataka leo mkabidhi nyaraka zenu na tuweze kuwahakiki ili kuweza kutambulika kwani kutambua ianweza kuwa sehemu moja ya kinga yako kwani mazingira ya kazi yenu ni rahisi sana kuwepokwa uvunjifu wa amani ni muhimu sana kufanya kazi na mamlaka zilizopo ili muwe salama na mnaowahudumia waweze kuwa salama pia.
Amesema wengi wao wanatumika kuvunja taratibu na wanatumika kutapeli na kuchukua mal za watu na kuzifanya mali yenu vitendo kama hiv vinawaumiza wananchi hivyo kama serkali hawatakuwa tayari kuona vitendo hivyo vy kuwanyanyasa wananchi vikiendelea kutokea.
"Lazima amri ya mahakama itekelezwe mimi nnachokipigania ni wananchi wanaoonewa, has kwa wale wanaotumia mgongo wa mahakama kuwanyonya wananchi wanyonge wanaotafuta haki zao hivyo kwa kutambulika kutasaidia kuondokana na wale wanaowanyanyasa wananchi wetu wa mkao huu."Amesema Rc Makonda.
Amesema zipo kampuni za udalali zinazofoji nakala za hukumu, mihuri, sahihi za mahakama,ofisi ya Mkoa, Wilaya na Mitaa na wakati mwingine kufanya minada bila kufuata taratibu.
Kwa upande wa Madalali waliofika katika kikao hicho wamemshukuru Makonda kwa uamuzi wa kuwatambua ili wapate ushirikiano wa Serikali kwakuwa wapo baadhi ya madalali waliokuwa wakifanya kazi hiyo kinyume na sheria na kuwachafulia kazi wale wenaofata taratibu za kazi hiyo.
Amesema zipo kampuni za udalali zinazofoji nakala za hukumu, mihuri, sahihi za mahakama,ofisi ya Mkoa, Wilaya na Mitaa na wakati mwingine kufanya minada bila kufuata taratibu.
Kwa upande wa Madalali waliofika katika kikao hicho wamemshukuru Makonda kwa uamuzi wa kuwatambua ili wapate ushirikiano wa Serikali kwakuwa wapo baadhi ya madalali waliokuwa wakifanya kazi hiyo kinyume na sheria na kuwachafulia kazi wale wenaofata taratibu za kazi hiyo.
Vilevile ameitaka ametoa Onyo kwa kampuni zinazofanya kazi ya kukamata Pikipiki (bodaboda) kwa mtindo wa kuvamia kitendo kinachohatarisha usalama wa Dereva na Abiria.
Amesema zipo baadhi ya kampuni zimekuwa zikivizia madereva wa Bodaboda kisha kuwavamia na kuwakamata na wakati huohuo kuwapiga kitendo ambacho amesema hawezi kukiruhusu kiendelee kwenye Mkoa wake.
Hivyo makala MAKONDA ASISITIZA MAKAMPUNI YA UDALALI KUFUATASHERIA ,WANAO KAMATA BODA BODA KWA KUWA PIGA WAONYWA
yaani makala yote MAKONDA ASISITIZA MAKAMPUNI YA UDALALI KUFUATASHERIA ,WANAO KAMATA BODA BODA KWA KUWA PIGA WAONYWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKONDA ASISITIZA MAKAMPUNI YA UDALALI KUFUATASHERIA ,WANAO KAMATA BODA BODA KWA KUWA PIGA WAONYWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/makonda-asisitiza-makampuni-ya-udalali.html
0 Response to "MAKONDA ASISITIZA MAKAMPUNI YA UDALALI KUFUATASHERIA ,WANAO KAMATA BODA BODA KWA KUWA PIGA WAONYWA"
Post a Comment