title : MAKATIBU MEZANI WA BUNGE WAPEWA MAFUNZO
kiungo : MAKATIBU MEZANI WA BUNGE WAPEWA MAFUNZO
MAKATIBU MEZANI WA BUNGE WAPEWA MAFUNZO
Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai akifungua mafunzo ya Makatibu mezani wa Bunge, Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo ya wiki moja yanatolewa chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia mradi wa pili wa kulijengea Bunge uwezo (LSP II). Kushoto kwa Katibu wa Bunge ni Spika Mstaafu wa Bunge, Mhe. Pius Msekwa ambaye ni mmojawapo wa watoa mada katika mafunzo hayo na Kulia kwa Katibu wa Bunge ni Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, Bi. Nenelwa Wankanga.
Spika Mstaafu wa Bunge Mhe. Pius Msekwa akizungumza wakati wa mafunzo ya Makatibu mezani wa Bunge. Mhe. Msekwa ni mmojawapo wa watoa mada katika mafunzo hayo ya wiki moja yanatolewa chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia mradi wa pili wa kulijengea Bunge uwezo (LSP II).
c. Mkurugenzi Mstaafu wa Shughuli za Bunge Ndg. Japhet Sagasii (aliyesimama) akitoa mada wakati wa mafunzo hayo ya Makatibu mezani wa Bunge. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mstaafu- Ofisi ya Bunge Ndg. Charles Mloka ambaye naye ni mtoa mada katika mafunzo hayo.
Spika Mstaafu wa Bunge Mhe. Pius Msekwa wa (pili toka kulia waliokaa), Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai (wa pili toka kushoto waliokaa) katika picha ya pamoja na washiriki wa Mafunzo ya Makatibu mezani wa Bunge maara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo Jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala MAKATIBU MEZANI WA BUNGE WAPEWA MAFUNZO
yaani makala yote MAKATIBU MEZANI WA BUNGE WAPEWA MAFUNZO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKATIBU MEZANI WA BUNGE WAPEWA MAFUNZO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/makatibu-mezani-wa-bunge-wapewa-mafunzo.html
0 Response to "MAKATIBU MEZANI WA BUNGE WAPEWA MAFUNZO"
Post a Comment