title : Dakika 30 ZA Huzuni wakati ASLAY ALIVYOWALIZA WATU ESCAPE ONE
kiungo : Dakika 30 ZA Huzuni wakati ASLAY ALIVYOWALIZA WATU ESCAPE ONE
Dakika 30 ZA Huzuni wakati ASLAY ALIVYOWALIZA WATU ESCAPE ONE
Na Humphrey Shao , Globu ya Jamii
Ilikuwa Usiku wa February 17 mwaka huu msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Aslay Isihaka alibadilisha historia ya muziki katika Maisha yake kwa kufanya shoo kubwa ya Mapenzi na Muimbaji Mwenzie Nandy ambae wameshirikiana katika nyimbo nyingi.
Licha ya usiku huo kufikiriwa kuwa wa nyimbo za Mahaba mambo yalikwenda tofauti kwa nusu saa nzima pale Aslaya alipopanda jukwaani na kibao cha “Angekuwepo” wimbo ambao aliumba kwa ajili ya kumkumbuka Mama yake Mzazi.
Aslay ambaye aliimba kisha kuishia kati na kwenda kumsogelea Mama Mzazi wa Nandy na kusema kuwa “natamani muda huu Mama yangu muda huu angekuwa hapa lakini sio mapenzi yangu...Natamani namimi ningekuwa kama Nandy naimba Mama yangu anaona. Hivyo nikuombe Mama Nandy kuanzia leo uwe mama yangu hili niweze kupata faraja kama anayopata mwanao” alisema Aslay.
Maneno yaliteka hisia za watu wengi na kumfanya Mama yake Nandy kuamka na kwenda kucheza na Aslay na kufanya watu wengi kuinuka kwenda kumwambia mwanamuziki huyo aendelee kuimba na kuacha kulia.
Aslay ambaye aliendelea kuimba wimbo huo huku akiwa amekaa chini kwa huzuni na kutengeneza simanzi kubwa ndani ya ukumbi wa Escape One kwa zaidi ya Dk 30. Wengi walilengwa na machozi na kukubali kuwa Mama ni wa muhimu kuliko kitu chochote maishani.
Aslay Isihaka akionyesha kidole juu kumshukuru Mungu kwa yote yaliyotekea katika maisha yake.
Aslay akimuomba Mama yake Nandy kuwa Mama yake wa kumlea wakati anaimba wimbo wake angekuwepo
Aslay akicheza na Mama yake Nandy mara baada ya kukubali kuwa Mama Mlezi
Mmoja wa Mashabiki wakinyamazisha Aslay asilie wakati anaimba wimbo angekuwepo
Mashabiki wa muziki wakiwa wamesimama kwa huzuni wakati Aslay akiimba wimbo huo
Hivyo makala Dakika 30 ZA Huzuni wakati ASLAY ALIVYOWALIZA WATU ESCAPE ONE
yaani makala yote Dakika 30 ZA Huzuni wakati ASLAY ALIVYOWALIZA WATU ESCAPE ONE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Dakika 30 ZA Huzuni wakati ASLAY ALIVYOWALIZA WATU ESCAPE ONE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/dakika-30-za-huzuni-wakati-aslay.html
0 Response to "Dakika 30 ZA Huzuni wakati ASLAY ALIVYOWALIZA WATU ESCAPE ONE"
Post a Comment