title : MAENEO YA KITALII YANAYOPATIKANA KUSINI MWA TANZANIA
kiungo : MAENEO YA KITALII YANAYOPATIKANA KUSINI MWA TANZANIA
MAENEO YA KITALII YANAYOPATIKANA KUSINI MWA TANZANIA
Miongoni mwa maeneo ya kitalii ambayo hayapewi kipaumbele au kutokuwa maarufu ni pamoja na Kusini mwa Tanzania. Tofauti na vivutio vya kitalii vya kanda ya Kaskazini kuwa maarufu kama vile Mlima Kilimanjaro, Hifadhi za Serengeti na Ngorongoro, kuna uwezekano mkubwa kwamba Kusini mwa Tanzania kuna hazina kubwa ya vivutio kwa watalii ambavyo havitangazwi au kuvumbuliwa na wengi.
Miongoni mwa sababu ambazo zimekuwa zikikwamisha shughuli za kitalii kwa ukanda wa Kusini ni pamoja na miundominu hafifu kama vile barabara, viwanja vya ndege ambavyo hupelekea maeneo hayo kufikika kwa ugumu pamoja na upungufu wa malazi kama vile hoteli za kisasa na zinazokidhi vigezo.
Kwa kutambua umuhimu wa ukanda huu, serikali ya awamu ya tano imekuwa ikifanya jitihada za makusudi ambazo zitakuwa ni chachu katika kukuza utalii. Jitihada hizo ni pamoja na kuzinduliwa kwa mpango wa uwekezaji katika miundombinu ya mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa Kusini mwa Tanzania (REGROW) eneo la Kihesa, Kilolo mkoani Iringa. Mradi huo ulizinduliwa hivi karibuni na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Bi. Samia Suluhu na kuhudhuriwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangala.
Pamoja na jitihada hizo watalii na watanzania kwa ujumla wanahitaji kujua vivutio vinavyopatikana katika eneo hilo. Kwa kutambua umuhimu wa kutoa elimu juu ya vivutio mbalimbali nchini Tanzania, Jumia Travel imekukusanyia vivutio na shughuli zifuatazo za kitalii pindi utembeleapo eneo la Kusini mwa Tanzania.
Iringa. Mkoa wa Iringa ni kivutio tosha kutokana na historia yake ndefu tangu enzi za utawala wa kikoloni wa Wajerumani. Ni eneo ambalo Wajerumani walijenga ngome yao kwa ajili ya kupambana na vuguvugu za harakati za kukataa kutawaliwa kutoka kwa kabila la Wahehe ambazo ziliongozwa na Chifu Mkwawa. Mji huu ambao ulijengwa tangu karne ya 19 una mambo mengi ya kujifunza na kujionea pindi utembeleapo ambayo hayapatikani sehemu yoyote nchini.
Isimila. Mbali na harakati za wazi za kupinga ukoloni wa Wajerumani, eneo la Kusini linasifika kwa kupatikana kwa mabaki ya historia za kale. Eneo hili limegundulika kuwa na masalia ya kutosha ya zana za kale za Zama za Chuma kuliko eneo lolote duniani, ambapo inasemekana ni maeneo ya mwanzo kabisa kuzalisha zana za viwandani na vichwa vya mishale.
Bonde la Kilombero. Ukubwa wa bonde hili ambalo hujaa maji kwa msimu umelifanya kuwa ndilo kubwa katika ukanda wa Afrika ya Mashariki. Kuna shughuli nyingi za kufanya kama mtalii na mambo kadhaa ya kujifunza pindi utembeleapo eneo hili linalopatikana mkoani Morogoro. Miongoni mwa shughuli za kufurahia ni pamoja na kujionea ndege wa aina mbalimbali wa kuvutia pamoja na shughuli za kijadi za wakazi wa eneo hilo kama vile uvuvi.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MAENEO YA KITALII YANAYOPATIKANA KUSINI MWA TANZANIA
yaani makala yote MAENEO YA KITALII YANAYOPATIKANA KUSINI MWA TANZANIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAENEO YA KITALII YANAYOPATIKANA KUSINI MWA TANZANIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/maeneo-ya-kitalii-yanayopatikana-kusini.html
0 Response to "MAENEO YA KITALII YANAYOPATIKANA KUSINI MWA TANZANIA"
Post a Comment