DKT. KIGWANGALLA AFANYA MAZUNGUMZO NA MUWAKILISHI BENKI YA DUNIA NCHINI

DKT. KIGWANGALLA AFANYA MAZUNGUMZO NA MUWAKILISHI BENKI YA DUNIA NCHINI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DKT. KIGWANGALLA AFANYA MAZUNGUMZO NA MUWAKILISHI BENKI YA DUNIA NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DKT. KIGWANGALLA AFANYA MAZUNGUMZO NA MUWAKILISHI BENKI YA DUNIA NCHINI
kiungo : DKT. KIGWANGALLA AFANYA MAZUNGUMZO NA MUWAKILISHI BENKI YA DUNIA NCHINI

soma pia


DKT. KIGWANGALLA AFANYA MAZUNGUMZO NA MUWAKILISHI BENKI YA DUNIA NCHINI

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na Muwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Daniel Mira-Salama ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa REGROW kwa ajili ya kusimamia maliasili na kuendeleza utalii wa Ukanda wa Kusini ofisini kwake mjini Dodoma leo Januari 06, 2018 ambapo wamejadili mambo mbalimbali ya kuboresha mradi huo wakati wa utekelezaji. 

Miongoni mwa mambo waliyojadili ni kuboresha miundombinu ya barabara kuunganisha maeneo ya vivutio na miji ya ukanda huo pamoja na viwanja vya ndege ndani ya hifadhi viwe na hadhi na ubora wa kutua ndege kubwa ikiwemo za Air Tanzania. 

"Nawapongeza kwa mradi huu ambao ni mzuri sana kwenye uhifadhi lakini una mapungufu kidogo kwenye biashara ya utalii jambo ambalo ni muhimu kuangaliwa ili uwe na tija zaidi kwa jamii na taifa kwa ujumla" alisema Dk. Kigwangalla.

Alimuomba mratibu huyo kuona namna ya kubadilisha vipengele vya utekelezaji wa mradi huo ili uweze kuwa na tija zaidi hususan suala la miundombinu ya kuunganisha hifadhi mbalimbali za ukanda huo na miji ili kurahisisha usafiri wa kufikia vivutio hivyo kwa muda mfupi na kwa wakati.

Kwa upande wake mratibu huyo alisema jambo hilo linajadilika na kwamba uendelezaji wa maeneo hayo ni mtambuka ukihusisha Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ambazo nazo zimeahidi kuboresha miundombinu ya maeneo hayo.

Mradi wa REGROW unatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 12 Februari mwaka huu Mjini Iringa na Mhe. Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan. Mwezi Agosti mwaka jana Serikali ya Tanzania ilisaini mkopo wa masharti nafuu wa Dola za Kimarekani Milioni 150 sawa na takriban bilioni 340 za Tanzania kwa ajili ya kuendeleza mradi huo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (katikati) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Muwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Daniel Mira-Salama ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa REGROW kwa ajili ya kusimamia maliasili na kuendeleza utalii wa Ukanda wa Kusini ofisini kwake mjini Dodoma leo Januari 06, 2018 ambapo wamejadili mambo mbalimbali ya kuboresha mradi huo wakati wa utekelezaji. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Aloyce Nzuki. 
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akimsikiliza Muwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Daniel Mira-Salama ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa REGROW kwa ajili ya kusimamia maliasili na kuendeleza utalii wa Ukanda wa Kusini ofisini kwake mjini Dodoma leo Januari 06, 2018 ambapo wamejadili mambo mbalimbali ya kuboresha mradi huo wakati wa utekelezaji. 
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akiagana na Muwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Daniel Mira-Salama ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa REGROW kwa ajili ya kusimamia maliasili na kuendeleza utalii wa Ukanda wa Kusini ofisini kwake mjini Dodoma leo Januari 06, 2018 baada ya kujadili mambo kadhaa ya kuboresha mradi huo wakati wa utekelezaji. Katikati ni Mratibu wa mradi huo kutoka Tanzania, Someni Mteleka. (PICHA NA HAMZA TEMBA-WMU)


Hivyo makala DKT. KIGWANGALLA AFANYA MAZUNGUMZO NA MUWAKILISHI BENKI YA DUNIA NCHINI

yaani makala yote DKT. KIGWANGALLA AFANYA MAZUNGUMZO NA MUWAKILISHI BENKI YA DUNIA NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DKT. KIGWANGALLA AFANYA MAZUNGUMZO NA MUWAKILISHI BENKI YA DUNIA NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/dkt-kigwangalla-afanya-mazungumzo-na.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DKT. KIGWANGALLA AFANYA MAZUNGUMZO NA MUWAKILISHI BENKI YA DUNIA NCHINI"

Post a Comment