title : BENKI YA EQUITY YAZINDUA HUDUMA YA EAZZYBANKING KURAHISISHA HUDUMA KWA WATEJA WAO BILA STRESS
kiungo : BENKI YA EQUITY YAZINDUA HUDUMA YA EAZZYBANKING KURAHISISHA HUDUMA KWA WATEJA WAO BILA STRESS
BENKI YA EQUITY YAZINDUA HUDUMA YA EAZZYBANKING KURAHISISHA HUDUMA KWA WATEJA WAO BILA STRESS
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii.
BENKI ya Equity imezindua huduma za kibenki kwa njia ya mtandao ambapo wateja wao sasa watapata huduma mahali popote kupitia simu za mkononi, tablets na kompyuta za mezani na mpakato.
Huduma hizo watazipata kupitia Eazzy Banking kwa kufanya miamala kirahisi iwe usiku au mchana, wakiwa nyumbani, au ofisini na kubwa zaidi sasa watakuwa na nafasi ya kuokoa muda na gharama.
Akizungumza Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Eazzy Banking, Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Joseph Iha amesema kuwa huduma hizo mpya zitatoa fursa kwa wateja kufanya miala mahali popote.
"Huduma za Eazzy Banking zitaambana na EazzyBanking App, app ya kimataifa ya masuala ya kifedha inayounganisha huduma za laini za simu na kuwawezesha wateja kutuma fedha na pia kufanya malipo kupitia simu zao popote walipo na wakati wowote.
"EazzyBanking ni rahisi kuianzisha na hutoa huduma za kipekee kama kutuma fedha kwenda akaunti za benki au mitandao ya simu, kuomba na kulipia mikopo , kulipia bili(ankara) na aina ya huduma za malipo," amesema Iha.
Wateja walihudhuria uzinduzi wa huduma ya Eazzy Banking inayotolewa na benki ya Equity jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Joseph Iha akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam kutoa ufafanuzi wa masuala mbali mbali mara baada ya uzinduzi wa huduma ya Eazzy Banking inayomsaidia mteja kufanya miamala yake bila stress wakati wowote 24/7 popote atakapokuwa. Pembeni ni wakurugenzi wa Bodi ya Benki hiyo ikiongozwa na Simbeye.
Hivyo makala BENKI YA EQUITY YAZINDUA HUDUMA YA EAZZYBANKING KURAHISISHA HUDUMA KWA WATEJA WAO BILA STRESS
yaani makala yote BENKI YA EQUITY YAZINDUA HUDUMA YA EAZZYBANKING KURAHISISHA HUDUMA KWA WATEJA WAO BILA STRESS Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BENKI YA EQUITY YAZINDUA HUDUMA YA EAZZYBANKING KURAHISISHA HUDUMA KWA WATEJA WAO BILA STRESS mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/benki-ya-equity-yazindua-huduma-ya.html
0 Response to "BENKI YA EQUITY YAZINDUA HUDUMA YA EAZZYBANKING KURAHISISHA HUDUMA KWA WATEJA WAO BILA STRESS"
Post a Comment