title : YANGA SC KUIVAA AZAM BILA WACHEZAJI WAKE SABA
kiungo : YANGA SC KUIVAA AZAM BILA WACHEZAJI WAKE SABA
YANGA SC KUIVAA AZAM BILA WACHEZAJI WAKE SABA
Na Agness Francis, Globu ya Jamii
MABINGWA Watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC kesho kukutanaa uso kwa uso na AzamFc katika kukamilisha mzunguko wa kwanza,mchezo utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.
Akizungumza Msemaji Mkuu wa Yanga SC Dismas Ten leo Katika Makao makuu yao amesema wachezaji wapo fiti kuelekea mpambano huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki kuwa wamejipanga kuondoka na ushindi dhidi ya Azam FC kuachilia mbali kuwa watakuwa wageni wa mchezo huo mashambulizi yatakuwa ya kutosha katika kuonesha uwezo mkubwa walionao.
Aidha amesema kikosi hicho kitawakosa wachezaji wake nyota katika mtanange huo ambao ni Thabani Kamusoko, Amiss Tambwe, Yoana Mkomola, Pato Ngonyani, Donald Ngoma, Abdalah Shaib ambao wako majeruhi pamoja na Pius Biswita ambaye anatumukia adhabu ya kadi 3 za njano.
Pia Msemaji Huyo amesema kuwa "katika mchezo wao wa kesho watamkosa Kocha Msaidizi shedrack Nsajigwa ambaye amepa msiba,"amesema Dismas.
Pia Dismas amesema kwa siku ya kesho Kocha Mkuu George Lwandamina atarejea katika benchi la ufundi kuongoza kikosi chake kama ilivyokuwa hapo awali ikiwa kibali chake kipo hatua za mwisho kukamilika
Mzambia huyo alikuwa akikaa jukwaani wakati wa mechi za Mabingwa hao zikichezwa kwa sababu ya kumalizika kwa muda wa kibali chake cha kufanya kazi hapa nchini.
Hivyo makala YANGA SC KUIVAA AZAM BILA WACHEZAJI WAKE SABA
yaani makala yote YANGA SC KUIVAA AZAM BILA WACHEZAJI WAKE SABA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala YANGA SC KUIVAA AZAM BILA WACHEZAJI WAKE SABA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/yanga-sc-kuivaa-azam-bila-wachezaji.html
0 Response to "YANGA SC KUIVAA AZAM BILA WACHEZAJI WAKE SABA"
Post a Comment