title : MWANAMKE WA KWANZA AAPISHWA KUWA MEJA JENERALI KENYA
kiungo : MWANAMKE WA KWANZA AAPISHWA KUWA MEJA JENERALI KENYA
MWANAMKE WA KWANZA AAPISHWA KUWA MEJA JENERALI KENYA
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
RAIS wa Kenya Uhuru Kenyata amemwapisha Fatuma Ahmed kuwa Meja Jenerali nchini humo na kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo.
Jenerali Ahmed anakuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo kwa kuwa msaidizi mkuu wa majeshi nafasi ambayo haikuwa kushikwa na mwanamke katika masuala ya ulinzi na usalama nchini humo.
Katika hafla hiyo Kenyata alieleza kuwa amemchagua ili awe kioo kwa wanawake nchini humo na kuthibitisha kuwa hakuna kinachoshindikana.
Aidha alieleza kufurahishwa na namna jeshi la Kenya linavyofanya kazi hasa katika kulihudumia taifa bila kujali dini, itikadi wala rangi, wamekuwa waaminifu katika kuhudumia taifa hilo lenye watu 42 milioni.
Naye Jenerali mteule amemshukuru Rais Kenyata kwa uteuzi huo na kueleza kuwa: "Ninafuraha sana kwa nafasi mpya niliyochaguliwa na inaonesha namna Rais anavyothamini mchango wa wanawake katika maendeleo ya taifa letu" alieleza Jenerali Fatuma.
Jenerali Fatma Ahmed alianza kushika kasi mwaka 2015 baada ya kuchaguliwa kuwa brigedia wa jeshi nafasi ambayo haikuwahi kushikwa na mwanamke nchini humo.
Jenerali Fatuma ametumikia jeshi la ulinzi la Kenya kwa zaidi ya miaka 30 kuanzia miaka ya 1983.
RAIS wa Kenya Uhuru Kenyata amemwapisha Fatuma Ahmed kuwa Meja Jenerali nchini humo na kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo.RAIS wa Kenya Uhuru Kenyata amemwapisha Fatuma Ahmed kuwa Meja Jenerali nchini humo na kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo.
Hivyo makala MWANAMKE WA KWANZA AAPISHWA KUWA MEJA JENERALI KENYA
yaani makala yote MWANAMKE WA KWANZA AAPISHWA KUWA MEJA JENERALI KENYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MWANAMKE WA KWANZA AAPISHWA KUWA MEJA JENERALI KENYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/mwanamke-wa-kwanza-aapishwa-kuwa-meja.html
0 Response to "MWANAMKE WA KWANZA AAPISHWA KUWA MEJA JENERALI KENYA"
Post a Comment