title : VYAMA VYA SIASA 38,WASHIRIKI ZAIDI YA 130 KUTOKA NJE YA AFRIKA KUSHIRIKI MKUTANO WA KIDUNIA ULIOANDALIWA NA CPC NA CCM JIJINI DAR ES SALAAM
kiungo : VYAMA VYA SIASA 38,WASHIRIKI ZAIDI YA 130 KUTOKA NJE YA AFRIKA KUSHIRIKI MKUTANO WA KIDUNIA ULIOANDALIWA NA CPC NA CCM JIJINI DAR ES SALAAM
VYAMA VYA SIASA 38,WASHIRIKI ZAIDI YA 130 KUTOKA NJE YA AFRIKA KUSHIRIKI MKUTANO WA KIDUNIA ULIOANDALIWA NA CPC NA CCM JIJINI DAR ES SALAAM
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kunatarajia kufanyika mkutano wa kidunia wa vyama vya siasa pamoja na kikao maalum cha Afrika ambapo zaidi ya washiriki 130 wanatarajia kushiriki mkutano huo utakaofanyika jiini Dar es Salaam.
Akizungumzia mkutano huo katika Ofisi Ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijini Dar es Salaam Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesema CCM imepata heshima kubwa ya mwenyeji wa mkutano huo wa kidunia.
Tunapenda kuujulisha umma wa watanzania kuwa tarehe 17-18 Julai 2018 kutafanyika Mkutano wa Kidunia wa Vyama vya Siasa, Kikao Maalum cha Afrika, Jijini Dar es Salaam. Mkutano huu utaleta zaidi ya vyama vya siasa 38 kutoka Afrika na zaidi ya washiriki 130 kutoka nje ya Afrika,"amesema.
Amefafanua mkutano huo umeandaliwa kwa ushirikiano wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kwamba mkutano huo ni sehemu ya matokeo mazuri ya utendaji kazi wa uongozi wa awamu ya tano ya Chama na Serikali chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais Dk.John Magufuli.
Pia amesema mkutano huo wa kihistoria na wa kwanza kufanyika Barani Afrika ni wapili kufanyika baada ya mkutano kama huo wa kidunia kufanyika Jijini Beijing, China Desemba mwaka 2017. Mkutano huo wa Desemba mwaka 2017 uliandaliwa na Chama Cha Kikomunisti Cha watu China (CPC) na Kiongozi Mwenyeji wa Mkutano huu alikuwa ni Kamaradi Xi Jinping Katibu Mkuu wa CPC na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China.
Polepole amesema kuwa mkutano huo utahudhuriwa pamoja na wajumbe wengine wa mkutano ni Kamaradi Song Tao Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha Watu wa China, Xu Luping Makamu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China na Kiongozi Mwenyeji wa Mkutano huu wa Kidunia wa Vyama vya Siasa ni Kamaradi John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hivyo makala VYAMA VYA SIASA 38,WASHIRIKI ZAIDI YA 130 KUTOKA NJE YA AFRIKA KUSHIRIKI MKUTANO WA KIDUNIA ULIOANDALIWA NA CPC NA CCM JIJINI DAR ES SALAAM
yaani makala yote VYAMA VYA SIASA 38,WASHIRIKI ZAIDI YA 130 KUTOKA NJE YA AFRIKA KUSHIRIKI MKUTANO WA KIDUNIA ULIOANDALIWA NA CPC NA CCM JIJINI DAR ES SALAAM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VYAMA VYA SIASA 38,WASHIRIKI ZAIDI YA 130 KUTOKA NJE YA AFRIKA KUSHIRIKI MKUTANO WA KIDUNIA ULIOANDALIWA NA CPC NA CCM JIJINI DAR ES SALAAM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/vyama-vya-siasa-38washiriki-zaidi-ya.html
0 Response to "VYAMA VYA SIASA 38,WASHIRIKI ZAIDI YA 130 KUTOKA NJE YA AFRIKA KUSHIRIKI MKUTANO WA KIDUNIA ULIOANDALIWA NA CPC NA CCM JIJINI DAR ES SALAAM"
Post a Comment