WILAYA YA CHEMBA YAANZA KUJIANDAA UZINDUZI WA SIKU YA MAADHIMISHO YA WANYAMA PORI DUNIANI.

WILAYA YA CHEMBA YAANZA KUJIANDAA UZINDUZI WA SIKU YA MAADHIMISHO YA WANYAMA PORI DUNIANI. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WILAYA YA CHEMBA YAANZA KUJIANDAA UZINDUZI WA SIKU YA MAADHIMISHO YA WANYAMA PORI DUNIANI., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WILAYA YA CHEMBA YAANZA KUJIANDAA UZINDUZI WA SIKU YA MAADHIMISHO YA WANYAMA PORI DUNIANI.
kiungo : WILAYA YA CHEMBA YAANZA KUJIANDAA UZINDUZI WA SIKU YA MAADHIMISHO YA WANYAMA PORI DUNIANI.

soma pia


WILAYA YA CHEMBA YAANZA KUJIANDAA UZINDUZI WA SIKU YA MAADHIMISHO YA WANYAMA PORI DUNIANI.

Na Shani Amanzi,

Uzinduzi wa kuelekea siku ya Maadhimisho ya Wanyama Pori Duniani Kitaifa, utafanyika Marchi 03, 2018 katika Mkoa wa Dodoma ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa na Wilaya ya Chemba imechaguliwa kuwa sehemu ya Uzinduzi wa Maadhimisho hayo kwa shughuli ya upandaji miti iliyofanyika katika kijiji cha Kelema Kuu ,tarehe 15 Januari, 2018.

Katika uzinduzi huo Mgeni Rasmi alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Chemba Ndugu. Nyakia Ally kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga.

Ndugu. Nyakia amesema, Jamii inatakiwa kuendelea kutunza mazingira kwa kupanda miti, sambamba na kutunza mazingira ya asili ya Wanyama Pori. Aliongeza kwa kusema zoezi la upandaji miti ni endelevu katika Wilaya ya Chemba na jumla ya miti elfu 2000 imepandwa katika kijiji cha Kelema Kuu kata ya Paranga, maeneo ya Taasisi na Makazi ya watu.

Wilaya ya Chemba imefanya shughuli ya upandaji miti katika Kijiji hicho kama sehemu ya kuunga mkono mkakati wa Serikali wa kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa wa kijani, sambamba na uhamasishaji wa utunzaji wa Wanyama pori kwa kuwa kijiji cha Kelema Kuu kinapakana na pori la akiba la Swagaswaga .

Pori la akiba Swaga swaga linatumika katika shughuli za Uwindaji wa Kitalii ambapo jamii inayozunguka pori hilo inanufaika kwa kupata mgao wa ruzuku unaotokana na shughuli za utalii.

Maadhimisho ya Uzinduzi wa siku ya Wanyama Pori Duniani umeshirikisha Katibu Tawala Wilaya ya Chemba Ndg. Nyakia Ally kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Chemba ,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt. Semistatus H. Mashimba, Mkurugenzi wa Taasisi ya Rafiki Wild Life Foundation, Wakuu wa Idara/Vitengo Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Viongozi wa Ngazi ya Kata, Kijiji na Wananchi. 
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Chemba Ndugu. Nyakia Ally kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga akizungumza mbele ya Wananchi (hawapo pichani) kuhusiana na ujio wa Uzinduzi wa kuelekea siku ya Maadhimisho ya Wanyama Pori Duniani Kitaifa, ambao unatarajiwa kufanyika Marchi 03, 2018 katika Mkoa wa Dodoma,huku Mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa,katika shughuli hiyo Wilaya ya Chemba imechaguliwa kuwa sehemu ya Uzinduzi wa Maadhimisho hayo kwa shughuli ya upandaji miti iliyofanyika katika kijiji cha Kelema Kuu ,tarehe 15 Januari, 2018.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Chemba Ndugu. Nyakia Ally kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga akishiriki upandaji miti kuelekea Uzinduzi wa siku ya Maadhimisho ya Wanyama Pori Duniani Kitaifa, ambao unatarajiwa kufanyika Machi 03, 2018 katika Mkoa wa Dodoma,huku Mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa.katika shughuli hiyo Wilaya ya Chemba imechaguliwa kuwa sehemu ya Uzinduzi wa Maadhimisho hayo kwa shughuli ya upandaji miti iliyofanyika katika kijiji cha Kelema Kuu ,tarehe 15 Januari, 2018.




Hivyo makala WILAYA YA CHEMBA YAANZA KUJIANDAA UZINDUZI WA SIKU YA MAADHIMISHO YA WANYAMA PORI DUNIANI.

yaani makala yote WILAYA YA CHEMBA YAANZA KUJIANDAA UZINDUZI WA SIKU YA MAADHIMISHO YA WANYAMA PORI DUNIANI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WILAYA YA CHEMBA YAANZA KUJIANDAA UZINDUZI WA SIKU YA MAADHIMISHO YA WANYAMA PORI DUNIANI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/wilaya-ya-chemba-yaanza-kujiandaa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WILAYA YA CHEMBA YAANZA KUJIANDAA UZINDUZI WA SIKU YA MAADHIMISHO YA WANYAMA PORI DUNIANI."

Post a Comment