WAZIRI MKUU AUVUNJA MFUKO WA WAKFU WA KUENDELEZA KAHAWA

WAZIRI MKUU AUVUNJA MFUKO WA WAKFU WA KUENDELEZA KAHAWA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MKUU AUVUNJA MFUKO WA WAKFU WA KUENDELEZA KAHAWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MKUU AUVUNJA MFUKO WA WAKFU WA KUENDELEZA KAHAWA
kiungo : WAZIRI MKUU AUVUNJA MFUKO WA WAKFU WA KUENDELEZA KAHAWA

soma pia


WAZIRI MKUU AUVUNJA MFUKO WA WAKFU WA KUENDELEZA KAHAWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuvunja Mfuko wa Wakfu wa Kuendeleza zao la Kahawa (CDTF) na amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuchunguza mwenendo wa mfuko huo tangu ulipoanzishwa.
Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Januari 14, 2018) wakati akizungumza na wadau wa zao hilo kwenye kikao cha kujadili maendeleo ya zao la kahawa alichokiitisha, mjini Dodoma. 
Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo baada ya kubaini kwamba uundwaji wa mfuko huo si wa kisheria bali ni wadau wa zao hilo kwa kushirikiana na Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB).
“Wakati Serikali inapambana kupunguza makato ya hovyo kwa wakulima, kumbe huku kuna chombo cha kuwachukulia fedha wakulima hii haikubaliki.”
Pia aliagiza kufungwa kwa ofisi za CDTF ili kupisha uchunguzi na baada ya CAG kukamilisha uchunguzi na kukabidhi ripoti, kazi zote zilizokuwa zinafanywa na mfuko huo zitafanywa na Bodi ya Kahawa.
Hata hivyo, Waziri Mkuu ameongeza kuwa  majukumu ya kuundwa kwa mfuko huo yanaingiliana na yale ya Bodi ya Kahawa, ambayo ni pamoja na kufuatilia maendeleo ya zao hilo, hivyo hakuna haja ya kuwa vyombo viwili vinavyofanya kazi moja.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu amepiga marufuku wanunuzi wa kahawa kwenda kununua kwa wanavijiji na badala yake kahawa yote itauzwa kwa njia ya minada.
“Kahawa itauzwa katika minada tu na utaratibu wa kutoa vibali kwa wanunuzi wa kahawa kwenda kununua kwa wananchi vijijini marufuku kuanzia sasa, kama kuna watu wamepeleka fedha zao wazirudishe kwani hazitafanya kazi.”
Amesema Wakuu wa Mikoa na Wilaya wasimamie uuzwaji wa zao hilo na kuwachukulia hatua wote watakaokutwa wananunua kahawa kwa wakulima. “Anayetaka kahawa akanunue mnadani na si kwa wanavijiji lengo ni kuhakikisha mkulima anapata tija.”
Pia ameziagiza halmashauri zote zinazolima kahawa nchini kuanzisha vitalu vya miche ya kahawa na kisha kuigawa bure kwa wakulima, pia Maofiza Kilimo wawaelimishe walkulima wote wenye miti mikongwe waanzisha mashamba mapya.
Kuhusu suala la utafiti wa zao hilo, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Kilimo itumie vyuo vyake vya kilimo ianzishe vituo vyake vya utafiti vitakavyofanya kazi ya utafiti wa zao hilo.


Hivyo makala WAZIRI MKUU AUVUNJA MFUKO WA WAKFU WA KUENDELEZA KAHAWA

yaani makala yote WAZIRI MKUU AUVUNJA MFUKO WA WAKFU WA KUENDELEZA KAHAWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU AUVUNJA MFUKO WA WAKFU WA KUENDELEZA KAHAWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/waziri-mkuu-auvunja-mfuko-wa-wakfu-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI MKUU AUVUNJA MFUKO WA WAKFU WA KUENDELEZA KAHAWA"

Post a Comment