title : PROF. KABUDI AMUWAKILISHA WAZIRI MKUU
kiungo : PROF. KABUDI AMUWAKILISHA WAZIRI MKUU
PROF. KABUDI AMUWAKILISHA WAZIRI MKUU
Leo Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Waziri wa Katiba na Sheria amemuwakilisha Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Ibada ya kuwekwa Wakfu Askofu wa Pili wa Dayosisi ya Shinyanga, Rev. Can. Capt. Johnson Japheth Chinyong’ole.
Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Stefano, Shinyanga na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Mheshimiwa George Huruma Mkuchika (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Viongozi wa Serikali ya Mkoa ikiongozwa na Mheshimiwa Josephine Matiro, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Viongozi wa Madhehebu mbalimbali ya Dini, Viongozi wa Vyama vya Siasa Mkoa wa Shinyanga na Waumini wa Dayosisi hiyo
Pamoja na kumpongeza kwa kuwekwa Wakfu, Mhe. Prof. Kabudi amemuomba Askofu Chinyong’ole awe kiungo thabiti baina ya waumini na kati ya waumini na Maaskofu katika kuzitatua changamoto zilizopo katika Kanisa na kwamba utumie vipawa na karama alizopewa na mwenyezi Mungu kuwaunganisha viongozi na waumini ili waweke mipango madhubuti ya kulijenga Kanisa na kuijenga Dayosisi ya Shinyanga.
Prof. Kabudi amemuhakikishia Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa Kanisa la Anglikana Tanzania katika ustawi wa Taifa kiroho, kisiasa, kiuchumi na kijamii na kwamba mchango huo umeiwezesha nchi yetu kupiga hatua katika nyanja zote; Kwamba Serikali itaendelea kushirikiana na madhehebu yote nchini katika kuweka misingi ya kila raia kuabudu kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Nchi.
Kabla ya kuchaguliwa Mwezi Oktoba, 2017 Askofu Chinyong’ole alikuwa Katibu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania kwa miaka mitatu. Askofu Chinyong’ole anakuwa Askofu wa Pili kuiongoza Dayosisi ya Shinyanga iliyoanzishwa Novemba, 2005 baada ya Dayosisi ya Victoria Nyanza kugawanywa.

Mhe. Prof. Palamagamba J. Kabudi (Mb) Waziri wa Katiba na Sheria akisoma hotuba wakati akimuwakilisha Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kuwekwa Wakfu Askofu wa Pili wa Dayosisi ya Shinyanga Rev. Can. Capt. Johnson Japheth Chinyong'ole.
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria akiwa kwenye picha ya pamoja na Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania mara baada ya kuwekwa Wakfu Askofu wa Pili wa Dayosisi ya Shinyanga Rev. Can. Capt. Johnson Japheth Chinyong'ole.
Pro. Kabudi akimpongeza Askofu wa Dayosisi ya Shinyanga Rev. Can. Capt. Johnson Japheth Chinyong'ole mara baada ya kuwekwa wakfu.
Hivyo makala PROF. KABUDI AMUWAKILISHA WAZIRI MKUU
yaani makala yote PROF. KABUDI AMUWAKILISHA WAZIRI MKUU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala PROF. KABUDI AMUWAKILISHA WAZIRI MKUU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/prof-kabudi-amuwakilisha-waziri-mkuu.html
0 Response to "PROF. KABUDI AMUWAKILISHA WAZIRI MKUU"
Post a Comment