TANESCO Yaaza Kuwabana Wadaiwa Sugu wa Bili za Umeme Jijini Dar es Salaam.

TANESCO Yaaza Kuwabana Wadaiwa Sugu wa Bili za Umeme Jijini Dar es Salaam. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TANESCO Yaaza Kuwabana Wadaiwa Sugu wa Bili za Umeme Jijini Dar es Salaam., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TANESCO Yaaza Kuwabana Wadaiwa Sugu wa Bili za Umeme Jijini Dar es Salaam.
kiungo : TANESCO Yaaza Kuwabana Wadaiwa Sugu wa Bili za Umeme Jijini Dar es Salaam.

soma pia


TANESCO Yaaza Kuwabana Wadaiwa Sugu wa Bili za Umeme Jijini Dar es Salaam.


Mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam, wakiwa na kifaa cha kukatia umeem, tayari kwa kazi kwenye transfoma ya kupeleka umeem kwenye eneo la kiwanda kinachomilikiwa na mfanyabishara maarufu jijini, Bw. Fida Hussein kilichiko Vingunguti leo Mei 4, 2017

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
“MANENO ni mawili tu “KA na TA” ukiunganisha Kata, asiyelipa kateni umeme” Hayo yalikuwa ni maneno ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, wakati akitoa hotuba ya uzinduzi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme mkoani Mtwara miezi michche iliyopita.
Kufuatia maagizo hayo ya Rais, Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa wake, Dkt. Tito Mwinuka, aliitisha mkutano na waandihi wa habari na kutoa ilani kwa wadaiwa wote “sugu” wa bili za umeme kuwa walipe madeni yao vinginevyo huduma ya umeme itasitishwa.
Baada ya tangazo hilo, baadhi ya taasisi za serikali likiwemo Jesho la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, kupitia kwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo, naye aliitisha mkutano na wanahabari na kueleza kuwa JWTZ italipa sdeni lake na kuagiza wahusika wafanye hivyo mara moja.
Leo hii Mei 4, 2017, Meneja wa TANESCO mkoa wa Ilala, Mhandisi Athanasius Nangali, aliwaita waandishi wa habari ofisini kwake na kuwaeleza kuwa taasisi za umma na binafsi zilizo katika mkoa wake, zilikuwa zikidaiwa jumla ya shilingi Bilioni 7, ambapo taasisi za serikali pekee zilikuwa na deni la  shilingi bilioni 6 na kwa sasa tayari zimelipa jumla ya shilingi bilioni 2 na kubaki deni la shilingi bikioni 4.
“Hizi taasisi za umma tumeingia nazo mkataba na kwakweli wameanza kulipa na tunaendelea kuwahimiza wafanye hivyo ili wasije kukosa huduma ya umeme.” Alisema Mhandisi Nangali.
Aidha alisema taasisi binafsi zinadaiwa shilingi Bilioni 1 na nyingi kati ya hizo hazijaingia mkataba wa malipo ya madeni yake na TANESCO kwa hivyo akatahadharisha kuwa TANESCO haitasita kuchukua hatua za kusitisha huduma ya umeme na kwa kuonyesha kuwa Shirika halifanyi mzaha, leo hii kampuni mbili moja ikimilikiwa na mfanyabiashara maarufu Fida Hussein iliyoko Vingunguti wilayani humo imesitishiwa huduma ya umeme kufuatia deni la shilingi Milioni 29.
Kampuni nyingine iliyoonja joto ya jiwe ni Iprintiliyoko eneo la Banda la Ngozi kandokando ya barabara ya Nyerere, kampuni hiyo hadi kufikia leo Mei 4, 2017 ilikuwa ikidaiwa jumla ya shilingi Milioni 16,95.
Maafisa wa TANESCO waliokuwa kwenye operesheni ya “kukata” umeme kwa wadaiwa sugu, walikuwa na stakabadhi zinazoonyesha kuwa kufikia leo Mei 4, 2017 kampuni hizo mbili zikikuwa zikidaiwa madeni hayo.  

 Mfanyakazi wa TANESCO kivaa gloves tayari kukata umeme
 Meneja wa TANESCO mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam, Mhandisi Athanasius Nangali, (kulia), akiwa na Afisa kutoka idara ya fedha TANESCO makao makuu, akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Mei 4, 2017.
 Mhandisi wa kudhibiti mapato TANESCO mkoa wa Ilala, Daniel Kimaro, akizungumza na waandishi baada ya kusitisha huduma ya umeme kwenye kampuni ya Iprint
 Hii ni stakabadhi ya leo Mei 4, 2017 ikionyesha kampuni ya I print ikidaiwa shilinhi milioni 16.95
 Baadhi ya wafanyakazi wa Iprint wakitafakari baada ya huduma ya umeme kusitishwa
 Maafisa wa TANESCO makao makuu, wakimsikiliza meneja wa kiwanda cha Fida Hussein(kulia)
 Wanahabari wakiwa kazini
Mhandisi Athanasius Nangali(kulia), akiongea na waandishi wa habari


Hivyo makala TANESCO Yaaza Kuwabana Wadaiwa Sugu wa Bili za Umeme Jijini Dar es Salaam.

yaani makala yote TANESCO Yaaza Kuwabana Wadaiwa Sugu wa Bili za Umeme Jijini Dar es Salaam. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TANESCO Yaaza Kuwabana Wadaiwa Sugu wa Bili za Umeme Jijini Dar es Salaam. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/tanesco-yaaza-kuwabana-wadaiwa-sugu-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TANESCO Yaaza Kuwabana Wadaiwa Sugu wa Bili za Umeme Jijini Dar es Salaam."

Post a Comment