title : WADAU WAJADILI MTAALA WA MAFUNZO KWA VYUO VYA USTAWI
kiungo : WADAU WAJADILI MTAALA WA MAFUNZO KWA VYUO VYA USTAWI
WADAU WAJADILI MTAALA WA MAFUNZO KWA VYUO VYA USTAWI
Kamishna Msaidizi Ustawi wa Jamii (Mafunzo) kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Bw. Simon Panga amesema utengenezaji mitaala ya taaluma ya Ustawi wa Jamii katika ngazi ya cheti na astashahada itasaidia kuboresha elimu ya ustawi wa jamii nchini.
Panga alisema hayo leo wakati akifungua mkutano wa siku moja wa wadau wa Ustawi wa Jamii kutengeneza mtaala wa Ustawi wa jamii kwa vyuo vinavyofundisha masuala ya Ustawi katika ngazi ya Cheti na astashahada leo jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kamishna Msaidizi Ustawi wa Jamii (Mafunzo), mtaala utakaopendekezwa na wadau utatumika na vyuo vyote Nchini tofauti na sasa ambapo kila chuo kinajitengenezea mtaala na utakuwa umepunguza majukumu na gharama kwa vyuo katika kutengeneza na kuandaa mitaala yao.
Kamishna Msaidizi Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawke na Watoto Simon Panga akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku moja wa wadau wa Ustawi wa Jamii kutengeneza mtaala wa Ustawi wa jamii kwa vyuo vinavyofundisha masuala ya Ustawi katika ngazi ya Cheti na Diploma jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Paulo Mwangozi akitoa ufafanuzi wakati wa wa mkutano wa siku moja wa wadau wa Ustawi wa Jamii kutengeneza mtaala wa Ustawi wa jamii kwa vyuo vinavyofundisha masuala ya Ustawi katika ngazi ya Cheti na Diploma jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya washiriki wa mkutano wa wadau wa Ustawi wa Jamii kutengeneza mtaala wa Ustawi wa jamii kwa vyuo vinavyofundisha masuala ya Ustawi katika ngazi ya Cheti na Diploma jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala WADAU WAJADILI MTAALA WA MAFUNZO KWA VYUO VYA USTAWI
yaani makala yote WADAU WAJADILI MTAALA WA MAFUNZO KWA VYUO VYA USTAWI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WADAU WAJADILI MTAALA WA MAFUNZO KWA VYUO VYA USTAWI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/wadau-wajadili-mtaala-wa-mafunzo-kwa.html
0 Response to "WADAU WAJADILI MTAALA WA MAFUNZO KWA VYUO VYA USTAWI"
Post a Comment