TAARIFA KWA UMMA KUHUSU USALAMA WA SEKTA YA KIBENKI NCHINI

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU USALAMA WA SEKTA YA KIBENKI NCHINI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TAARIFA KWA UMMA KUHUSU USALAMA WA SEKTA YA KIBENKI NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TAARIFA KWA UMMA KUHUSU USALAMA WA SEKTA YA KIBENKI NCHINI
kiungo : TAARIFA KWA UMMA KUHUSU USALAMA WA SEKTA YA KIBENKI NCHINI

soma pia


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU USALAMA WA SEKTA YA KIBENKI NCHINI

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuutaarifu umma kuwa taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusu sekta ya kibenki nchini kutokuwa salama si sahihi na zinapaswa kupuuzwa. Sekta ya kibenki nchini ipo salama na Benki Kuu ipo makini kuhakikisha kuwa sekta ya kibenki na mfumo wa fedha kwa ujumla ni salama na stahimilivu.

 Benki Kuu inaendelea kuzisimamia benki zote kwa ukaribu kama inavyotakiwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006. Taarifa zinazosambaa kuhusu kufungwa kwa benki zenye viwango vikubwa vya mikopo chechefu (non-performing loans) hazina ukweli wowote. Taarifa hizo zina lengo la kupotosha umma na kusababisha taharuki kwa wananchi. Benki Kuu inawakumbusha wananchi kuwa benki ndiyo sehemu salama ya kuhifadhi fedha zao. 

Benki Kuu inapenda kuuhakikishia umma kuwa haina lengo la kufuta leseni za benki bila sababu za msingi kama inavyopotoshwa kwenye mitandao ya kijamii. Ni lengo la Benki Kuu kuona kuwa benki zote zilizopewa leseni zinafanya vizuri. Aidha, ieleweke kuwa Benki Kuu hufuta leseni ya benki pale tu benki husika inaposhindwa kuzingatia vigezo ambavyo vimewekwa kisheria. Miongoni mwa sababu za msingi zinazoweza kusababisha kufutwa kwa leseni ya benki ni kuwa na mtaji chini ya kiwango kinachotakiwa kisheria, upungufu wa ukwasi na ukiukwaji wa sheria mbalimbali za kibenki, na si vinginevyo.

 Benki Kuu itaendelea kusimamia shughuli za kibenki kwa ukaribu na kwa mujibu wa Sheria ili kuhakikisha amana za wateja zinakuwa salama muda wote. Hivyo, wananchi wanaombwa kuwa na utulivu na kuondokana na taharuki inayosababishwa na watu wachache. Pia Benki Kuu inawakumbusha wananchi kutoziamini taarifa zisizo rasmi kuhusu usalama wa sekta ya kibenki nchini Tanzania. 

Taarifa rasmi kuhusu sekta ya kibenki hutolewa na Benki Kuu ya Tanzania ambayo kisheria ndiyo msimamizi wa sekta hiyo nchini. Wananchi wanakumbushwa kuwa usambazaji wa taarifa zisizo rasmi ni kinyume cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 na hatua kali zitachukuliwa kwa atakayebainika kufanya hivyo.

 Imetolewa na: Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki
 info@bot.go.tz
 Januari 9, 2018 
 BENKI KUU YA TANZANIA


Hivyo makala TAARIFA KWA UMMA KUHUSU USALAMA WA SEKTA YA KIBENKI NCHINI

yaani makala yote TAARIFA KWA UMMA KUHUSU USALAMA WA SEKTA YA KIBENKI NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TAARIFA KWA UMMA KUHUSU USALAMA WA SEKTA YA KIBENKI NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/taarifa-kwa-umma-kuhusu-usalama-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TAARIFA KWA UMMA KUHUSU USALAMA WA SEKTA YA KIBENKI NCHINI"

Post a Comment