Trend Solar kuwafikia wananchi washio kijijini

Trend Solar kuwafikia wananchi washio kijijini - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Trend Solar kuwafikia wananchi washio kijijini, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Trend Solar kuwafikia wananchi washio kijijini
kiungo : Trend Solar kuwafikia wananchi washio kijijini

soma pia


Trend Solar kuwafikia wananchi washio kijijini

Kampuni ya Trend Solar leo imezindua programu ya kisasa ya umeme ambayo itasaidia jamii kubwa ya waafrika waishio vijijini. Trend Solar ilianza huduma yake mwaka 2017, chini ya waasisi wake Irfan Mirza na Matt Tam ambao hubuni, kusambaza na pia hufadhili miradi ya umeme wa jua ambayo inalenga kuwafikia wakazi wenye kipato cha chini na maeneo ambayo umeme wa gridi haujafika.

Katika kipindi cha majaribio Trend Solar wameweza kuuza zaidi ya seti 500 kutoka kwenye maduka yao Dar es Salaam, Geita na Bagamoyo, na sasa kampuni hiyo itaongeza vifaa zaaidi Afrika Mashariki nzima ili kulifikia soko la umeme wa jua linalokadiriwa kufikia thamani ya dola za kimarekani Bilioni 3.1 barani Afrika.

Akizungumza katika uzinduzi, mwanzilishi na Mkurugenzi wa Trend Solar Bw. Irfan Mirza alisema “Kupitia Trend Solar tunawaondolea watu wetu tatizo la kusahaulika kwenye maendeleo ya kidigitali kwa kuwapatia simu ya gharama nafuu + intaneti ya bure + na vifaa vya kuchajia nyumbani. Tunaboresha zaidi biashara ya upatikanaji wa umeme mbadala na intaneti kwa kuwa kampuni ya kwanza duniani kuunganisha Simu na mfumo wa solar za majumbani (SHS).

“Katika kipindi cha majaribio tumepokea mrejesho mzuri zaidi ya tulivyotegemea na hasa baada ya kuongeza Simu janja yetu ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa watumiaji, ambao hawakuwa na njia ya kupata intaneti hapo awali. Sasa tuko katika nafasi nzuri ya kuwafikia watu milioni 36 ambao hawapati umeme wa gridi nchini Tanzania na kuwapa fursa zaidi kunufaika na maendeleo ya kidigitali”. Aliongeza Bw. Irfan.
Balozi wa Uingereza nchini Sarah Cooke akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa wakati wa  uzinduzi wa programu ya kisasa ya umeme ambayo itasaidia jamii kubwa ya waafrika waishio vijijini wakati wa kuingia mkataba wa Maudhui na Kampuni ya StarTimes.

Balozi wa Uingereza nchini Sarah Cooke(wa pili kulia) akizindua programu ya kisasa ya umeme wa nguvu ya Jua ambapo kampuni ya Trend Solar wameingia mkataba wa Maudhui na Kampuni ya StarTimes ambao ndio mtoa huduma wa matangazo ya kidigitali mwenye watumiaji wengi zaidi barani Afrika ikiwa na watumiaji zaidi ya Milioni 10.
Mkurugenzi wa Masoko wa Startimes, Li Kun(kushoto) akimkabidhi mpira Balozi wa Uingereza nchini Sarah Cooke mara baaada ya kuzindua  programu ya kisasa ya umeme ambayo itasaidia jamii kubwa ya waafrika waishio vijijini kati ya Trend Solar na Startimes Tanzania.
Picha ya pamoja


Hivyo makala Trend Solar kuwafikia wananchi washio kijijini

yaani makala yote Trend Solar kuwafikia wananchi washio kijijini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Trend Solar kuwafikia wananchi washio kijijini mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/trend-solar-kuwafikia-wananchi-washio.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Trend Solar kuwafikia wananchi washio kijijini"

Post a Comment