title : MBUNGE LUSHOTO AWATAKA MAAFISA UGANI KUACHA KUKAA OFISINI
kiungo : MBUNGE LUSHOTO AWATAKA MAAFISA UGANI KUACHA KUKAA OFISINI
MBUNGE LUSHOTO AWATAKA MAAFISA UGANI KUACHA KUKAA OFISINI
MAAFISA Ugani wa Kata na Vijiji wilayani Lushoto mkoani Tanga wametakiwa kuacha tabia ya kukaa ofisini badala yake wahakikisha wanakwenda kwa wakulima ili kuwapa elimu ya namna ya kulima kilimo cha kisasa ambacho kitakuwa na tija kwao hali itakayosaidia kuongeza uzalishaji wa mazao yao.
Kauli hiyo ilitolewa na Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia wakati wa ziara yake wa kuwatembelea wananchi katika vijiji mbalimbali iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kujikita kwenye shughuli za uzalishaji na kusikiliza kero zinazowakabili.
Akiwa kwenye kijiji cha Lwandai Kata ya Mlola, Mbunge huyo alisema wapo baadhi ya maafisa ugani wamekuwa wakikaa ofisini badala ya kwenda wa wananchi ambao wanajishughulisha na kilimo ili waweze kuwapa elimu ya namna ya kulima kisasa jambo ambalo limekuwa likichangia kurudisha maendeleo yao nyuma.
“Ndugu zangu maafisa ugani tambueni kuwa mnajukumu kubwa la kuhakisha mnakwenda kwa wananchi kuwaelimisha juu ya kulima kilimo chenye tija kwao kwani hiyo itawasaidia kuweza kupata mafanikio kuliko wanavyofanya sasa lakini pia acheni kukaa ofisini “Alisema.
“Kwani elimu ambayo mnaweza kuitoa inaweza kuwa chachu ya wakulima kuweza kulima mazao mazuri yatakayokuwa ya ushindani na soko la kisasa hivyo jambo hilo ni muhimu sana “Alisema.
Hivyo makala MBUNGE LUSHOTO AWATAKA MAAFISA UGANI KUACHA KUKAA OFISINI
yaani makala yote MBUNGE LUSHOTO AWATAKA MAAFISA UGANI KUACHA KUKAA OFISINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MBUNGE LUSHOTO AWATAKA MAAFISA UGANI KUACHA KUKAA OFISINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/mbunge-lushoto-awataka-maafisa-ugani.html
0 Response to "MBUNGE LUSHOTO AWATAKA MAAFISA UGANI KUACHA KUKAA OFISINI"
Post a Comment