title : JALADA KESI YA MHASIBU MKUU WA TAKUKURU NA WENZAKE LAPELEKWA TAKUKURU KWA UPELELEZI ZAIDI
kiungo : JALADA KESI YA MHASIBU MKUU WA TAKUKURU NA WENZAKE LAPELEKWA TAKUKURU KWA UPELELEZI ZAIDI
JALADA KESI YA MHASIBU MKUU WA TAKUKURU NA WENZAKE LAPELEKWA TAKUKURU KWA UPELELEZI ZAIDI
Upande wa mashtaka katika kesi ya utakatishaji fedha na kumiliki mali zisizoendana na kipato chake inayomkabili Mhasibu Mkuu wa Takukuru Godfrey Gugai na wenzake watatu umeiEleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa jalada la kesi hiyo limepelekwa Takukuru kwa ajili ya upelelezi zaidi.
Wakili wa Serikali Simon Wankyo akisaidiana na wakili Salim Msemo ameeleza leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati shauri hilo lilipofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa upelelezi ikiwa haujakamilika
Wakili Wankyo amedai, jalada la kesi hiyo lilipelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini(DPP) kwa ajili ya kusomwa na sasa limerudishwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) kwa ajili ya upelelezi zaidi.Ameongeza, baada ya kukamilisha upelelezi, jalada hilo litarudishwa tena kwa DPP ili kujiridhisha kama maelekezo aliyoyatoa yamefanyiwa Kazi.
Hata hivyo, baada ya maelezo hayo, wakili wa Utetezi Alex Mshumbusi alidai kuwa hategemei upelelezi kuchukua muda mrefu kwa sababu mshtakiwa Gugai alikuwa mtumishi wa Takukuru na tayari alishashtakiwa kinidhamu na Takukuru yenyewe na kupoteza ajira yake.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 31, mwaka huu itakapotajwa.
Mbali na Gugai, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasini Katera.Washitakiwa hao wanaokabiliwa na mashitaka 43 yakiwemo 20 ya utakatishaji fedha haramu, kumiliki mali zisizoendana na kipato na kughushi mikataba ya mauziano ya viwanja katika maeneo mbalimbali.
Katika shitaka la kwanza ambalo ni kumiliki mali ambazo hazina maelezo ambalo linamkabili Gugai, inadaiwa kati ya January 2005 na December 2015, jijini Dar es Salaam, akiwa ofisa wa umma ameajiriwa na TAKUKURU anamiliki mali zenye thamani zaidi ya Sh 3.6bilioni ambazo haziendani na kipato chake cha sasa wala cha nyuma.
Hivyo makala JALADA KESI YA MHASIBU MKUU WA TAKUKURU NA WENZAKE LAPELEKWA TAKUKURU KWA UPELELEZI ZAIDI
yaani makala yote JALADA KESI YA MHASIBU MKUU WA TAKUKURU NA WENZAKE LAPELEKWA TAKUKURU KWA UPELELEZI ZAIDI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JALADA KESI YA MHASIBU MKUU WA TAKUKURU NA WENZAKE LAPELEKWA TAKUKURU KWA UPELELEZI ZAIDI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/jalada-kesi-ya-mhasibu-mkuu-wa-takukuru.html
0 Response to "JALADA KESI YA MHASIBU MKUU WA TAKUKURU NA WENZAKE LAPELEKWA TAKUKURU KWA UPELELEZI ZAIDI"
Post a Comment