MRADI WA UMEME WA MAKAMBAKO-SONGEA KUNUFAISHA MIJI NA VIJIJI 191

MRADI WA UMEME WA MAKAMBAKO-SONGEA KUNUFAISHA MIJI NA VIJIJI 191 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MRADI WA UMEME WA MAKAMBAKO-SONGEA KUNUFAISHA MIJI NA VIJIJI 191, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MRADI WA UMEME WA MAKAMBAKO-SONGEA KUNUFAISHA MIJI NA VIJIJI 191
kiungo : MRADI WA UMEME WA MAKAMBAKO-SONGEA KUNUFAISHA MIJI NA VIJIJI 191

soma pia


MRADI WA UMEME WA MAKAMBAKO-SONGEA KUNUFAISHA MIJI NA VIJIJI 191

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MAKAMBAKO

KUKAMILIKA kwa Mradi wa ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovolti 220kV, na usambazaji umeme vijijini kutoka Makambako-Songea kupitia Njombe, unatarajiwa kuondoa kabisa tatizo la upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi wa mijini na vijiji vipatavyo 191, Meneja wa Mradi huo Mhandisi Didas Liyamuya,(pichani juu), amesema leo Jumanne Oktoba 10, 2017 wakati wa ziara ya Wahariri wa vyombo vya habari nchini.

Sambamba na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme pia utahusisha upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Makambako cha msongo wa umeme wa kilovolti 220/132/33Kv, na ujenzi wa vituo vingine vipya viwili, vya Madaba na Songea vya msongo umeme wa kilovolti 220/33kV, halikadhalika ujenzi wa mfumo wa usambazaji umeme wa msongo wa kilovoti 33 pamoja na kuunganisha wateja 22,700, katika mikoa hiyo alisema Mhandisi Liyamuya.

Akifafanua zaidi, katika mkoa wa Njombe, umeme utasambazwa katika maeneo ya Makambako na viunga vyake, Njombe yenyewe, na Ludewa, wakati mkoa wa Ruvuma umeme utasambazwa katika mji wa Songea na vijiji vilivyo katika wilaya ya Mbinga, Namtumbo na Madaba, na kuongeza kuwa umeme utakuwa wa msongo wa kilovolti 33 pamoja na ujenzi wa mawasiliano “OPGW”.

“Lengo la mradi huu ambao unafadhiliwa na Serikali ya Swedena kupitia Shirika lake la Misaada ya Kimaendeleo SIDA, Serikali ya Tanzania na Shirika la Umeme Nchini, TANESCO, ni kuboresha hali ya upatikanaji umeme katika maeneo ya uzalishaji na majumbani.” Alifafanua.
Mmoja wa wakazi wa kitongoji cha Lyamkena, mji wa Makambako mkoani Njombe, ambaye ni mteja mpya wa TANESCO, Bw.Thomas Kiwale, (kulia), akihakikiwa wakati wa zoezi la kuwahakiki wateja walioomba kuunganishiwa umeme kwenye eneo hilo, na afisa wa TANESCO, Bi.Atuokoe Mhingi, Oktoba 10, 2017
Wahariri na mafundi wa TANESCO, wakipita chini ya moja ya transofa zinazoednelea kufungwa kwenye mji wa Makambako Oktoba 10, 2017.
Moja ya minara ya kusafirisha umeme wa 220kV. ambao tayari umejengwa nje kidogo ya mji wa Makambako.
Kazi ya ujenzi wa msingi wa kufunga mitambo kwenye eneo la upanuzi wa kituo cha kupoza umeme wa 220kV Makambako ikiendelea.



Hivyo makala MRADI WA UMEME WA MAKAMBAKO-SONGEA KUNUFAISHA MIJI NA VIJIJI 191

yaani makala yote MRADI WA UMEME WA MAKAMBAKO-SONGEA KUNUFAISHA MIJI NA VIJIJI 191 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MRADI WA UMEME WA MAKAMBAKO-SONGEA KUNUFAISHA MIJI NA VIJIJI 191 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/mradi-wa-umeme-wa-makambako-songea.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MRADI WA UMEME WA MAKAMBAKO-SONGEA KUNUFAISHA MIJI NA VIJIJI 191"

Post a Comment