WANAMICHEZO 500 KUSHIRIKI MICHEZO YA WALEMAVU ‘RAIS SHEIN,MAMA SAMIA WAGENI RASMI’.

WANAMICHEZO 500 KUSHIRIKI MICHEZO YA WALEMAVU ‘RAIS SHEIN,MAMA SAMIA WAGENI RASMI’. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WANAMICHEZO 500 KUSHIRIKI MICHEZO YA WALEMAVU ‘RAIS SHEIN,MAMA SAMIA WAGENI RASMI’., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WANAMICHEZO 500 KUSHIRIKI MICHEZO YA WALEMAVU ‘RAIS SHEIN,MAMA SAMIA WAGENI RASMI’.
kiungo : WANAMICHEZO 500 KUSHIRIKI MICHEZO YA WALEMAVU ‘RAIS SHEIN,MAMA SAMIA WAGENI RASMI’.

soma pia


WANAMICHEZO 500 KUSHIRIKI MICHEZO YA WALEMAVU ‘RAIS SHEIN,MAMA SAMIA WAGENI RASMI’.


Tokeo la picha la picha ya uwanja wa taifa wa zanzibar

NA MWANDISHI WETU – ZANZIBAR
ZANZIBAR itakuwa mwenyeji wa michezo ya watu wenye ulemavu wa akili inayotarajia kuanza Desemba 7-10 katika uwanja wa Amaan ulioko Zanzibar.
Katika harakati za kuelekea mashindano hayo ya Taifa yanayotarajia wanamichezo 525 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini wakiwemo wenyeji.
Michezo hiyo ya walemavu itashirikisha michezo ya soka, Wavu na Riadha ambayo itachezwa katika mfumo wa michezo jumuishi ambayo inashirikisha watu wenye ulemavu wa akili na wasio na matatizo hayo, lengo likiwa ni kuachana na unyanyapaa ndio maana wanacheza timu moja.
Mfano kwenye timu moja ya soka, wachezaji saba ni wazima na wanne wanakuwa ni walemavu wa akili.
Baada ya michezo hiyo ya Zanzibar, Tanzania inatarajia kushiriki michezo ya dunia inayotarajia kufanyika mwakani nchini Abu Dhabi.
SOT nini watafanya?
Kuelekea katika michezo hiyo Kamati ya Olimpiki Maalum (SOT) ambayo ndiyo wasimamizi imejipanga na matukio kadhaa kuelekea michezo hiyo kwa kuanza kuwapokea na kuwapeleka Zanzibar kwenye michezo hiyo.
SOT watapokea wanamichezo 450 kutoka mikoa mbalimbali wakiwa na makocha wao 75 ambao wanatarajia kuwapokea Desemba 5 na kuwapa mapumziko ya saa kadhaa ambayo yatakuwa katika Jeshi la Wokovu Kurasini kabla ya saa chache kuelekea bandarini kwa ajili ya safari ya Zanzibar kwa meli ya Sealink.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa SOT, Dk. Juma Mwanandi Mwankemwa  Desemba 6, wanamichezo hao pamoja na makocha wao watatembelea vivutio vya utalii vilivyoko Zanzibar huku na kugaiwa vifaa vya ushiriki Desemba 7 itakuwa ni siku michezo hiyo kuanza.
Dk. Mwankemwa anasema michezo hiyo itafunguliwa Desemba 7, kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar ambako kabla ya michezo hiyo kuna baadhi ya taratibu ambazo wameziweka bayana kati yao na wenyeji Zanzibar ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mashindano hayo.
Anasema mikoa yote imeshapata taarifa za ushiriki wa michezo hiyo ambayo itagharamiwa na SOT kuanzia Jeshi la Wokovu  hadi mwisho wa mashindano hayo.
Makamu Mwenyekiti wa SOT, Mohamed Mwinyi Ramadhani anasema wamefanikisha suala la malazi kwa wanamichezo wote ambako wanamichezo watalala katika shule za Mwanakwerekwe C na Urafiki .
Ramadhani anasema watafanya ukarabati kidogo katika shule hizo wiki moja kabla ya michezo hiyo ndio watafanya marekebisho hayo ili wanafunzi walale katika maeneo salama.
Anasema kutakuwa na mabasi matano na Canter moja ambako pia kutakuwa na gari la wagonjwa  (Ambulance).
Michezo hiyo iitangaze Zanzibar
Mjumbe wa Bodi ya Olimpiki Maalum Zanzibar, Saada Hamad Ali anapendekeza kwamba ujio wa michezo hiyo kisiwani humo ni kukitangaza kisiwa hicho kiutalii kwa kuongeza watalii zaidi kwa sababu Zanzibar kuna maeneo ya kihistoria.
SOT wakutana na wenyeji  Zanzibar Novemba 7
Wajumbe watano wa Bodi ya  SOT ilikutana kwa mikutano kadhaa na kamati ya maandalizi ya Zanzibar, mkutano wa kwanza ulifanyika kati ya Kamati hizo mbili na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed  Mahmoud ambaye ndiye mwenyeji wa michezo hiyo.
Katika mazungumzo hayo, Mahmoud anasema yapo masuala ambayo wameshayazungumza na Kamati ya Zanzibar kwa lengo la kuweka sawa michezo hiyo kufanyika kwa ufanisi.
Mahmoud anasema anakubaliana na mfumo wa kuunda kundi la Wassap kwa ajili ya kufikia mafanikio ya michezo hiyo ambayo itakuwa na idadi kubwa ya washiriki .
Rais Shein mgeni rasmi katika ufunguzi
Katika mikakati ya kufanikisha michezo hiyo, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi utakaofanyika Desemba 7  huku kukiwa na matukio mengine mbalimbali.
Samia Suluhu mgeni rasmi ufungaji
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan Desemba 10 anatarajia kufunga michezo hiyo.
Kamati za maandalizi zaundwa BTMZ
Baada ya kikao na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Kikao kingine kilifanyika katika ofisi za Baraza la Michezo Zanzbar  (BTMZ) lililoko chini ya Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo, kikao kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa baraza hilo, Khamis Ali Mzee.
Katika mkutano huo, ziliundwa kamati saba kwa ajili ya kufanikisha michezo hiyo zikiwemo Ufundi, Mapokezi, Chakula, Afya, Ulinzi na Usalama, usafiri na Habari na Uenezi.
Kamati ya Ufundi inaundwa na Tifli Mustafa Nahoda, Mkurugenzi wa SOT Charles Ray, Omar Bakar na Lightess Mbilla huku Kamati ya Mapokezi inaundwa na wajumbe Abdallah Mohamed Ali, Mussa Abdul Rabi, Abdallah Hassan Ali na Salama Mohamed Ame huku Kamati ya Chakula inaundwa na Saada Hamad Ali, Kondo Ramadhani Karume, Amour Ali Khamis na Nassor Idrissa.
Kamati ya Afya inaundwa na Dk. Khatib Juma Bai, Dk Juma Mwanandi Mwankemwa, Kamati ya Ulinzi na Usalama inaundwa na Seif Haji Ame, Haidar Madowea na Zainab Omar Mtuli, Kamati ya Usafiri inaundwa na Abdul Wahab Dau, Juma Ali Juma na Usi Heri Chimbeni.
Kamati ya Habari na Uenezi inaundwa na Eshe Hamad Ali, Mohamed Mwinyi, Makuburi Ally, Salum Vuai na Abubakar Khatib Haji .
Ngoma ya Kibati kusindikiza michezo
Michezo hiyo itakayoshirikisha wadau mbalimbali wa michezo, itasindikizwa na Ngoma ya asili yak visiwani, Kibati. 


Hivyo makala WANAMICHEZO 500 KUSHIRIKI MICHEZO YA WALEMAVU ‘RAIS SHEIN,MAMA SAMIA WAGENI RASMI’.

yaani makala yote WANAMICHEZO 500 KUSHIRIKI MICHEZO YA WALEMAVU ‘RAIS SHEIN,MAMA SAMIA WAGENI RASMI’. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WANAMICHEZO 500 KUSHIRIKI MICHEZO YA WALEMAVU ‘RAIS SHEIN,MAMA SAMIA WAGENI RASMI’. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/wanamichezo-500-kushiriki-michezo-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WANAMICHEZO 500 KUSHIRIKI MICHEZO YA WALEMAVU ‘RAIS SHEIN,MAMA SAMIA WAGENI RASMI’."

Post a Comment