“VIONGOZI WA DINI WASIKATISHE TAMAA WAUMINI KUKABILI UKIMWI”- DK. MABOKO

“VIONGOZI WA DINI WASIKATISHE TAMAA WAUMINI KUKABILI UKIMWI”- DK. MABOKO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa “VIONGOZI WA DINI WASIKATISHE TAMAA WAUMINI KUKABILI UKIMWI”- DK. MABOKO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : “VIONGOZI WA DINI WASIKATISHE TAMAA WAUMINI KUKABILI UKIMWI”- DK. MABOKO
kiungo : “VIONGOZI WA DINI WASIKATISHE TAMAA WAUMINI KUKABILI UKIMWI”- DK. MABOKO

soma pia


“VIONGOZI WA DINI WASIKATISHE TAMAA WAUMINI KUKABILI UKIMWI”- DK. MABOKO

VIONGOZI wa madhehebu mbalimbali ya kidini wameombwa kusaidia kuondoa unyanyapaa wa wagonjwa wa Ukimwi ikiwa ni sehemu kamili ya kukabiliana na janga hilo nchini. Aidha wametakiwa kutumia program mbalimbali walizonazo katika mahubiri na kazi zao kuhakikisha kwamba taifa haliwi na maambukizi mapya ya Ukimwi na wale waliokuwa nao wanathaminika.
 Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko katika mkutano wa kuimarisha uratibu wa Afua za Ukimwi katika Taasisi za Kidini uliofanyika Chuo cha Maendeleo na Uongozi wa Elimu (ADEM) Bagamoyo. Alisema wakati taifa linapata maambukizi mapya 81,000 kwa mwaka, si sahihi kwa viongozi hao wa kidini kuupambanisha ugonjwa huo na mshahara wa dhambi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko akizungumza wakati akifungua mkutano wa kuimarisha uratibu wa Afua za Ukimwi katika Taasisi za Kidini uliofanyika Chuo cha Maendeleo na Uongozi wa Elimu (ADEM) Bagamoyo.(Picha zote na The Beautytz)
Alisema pamoja na ukweli kuwa mshahara wa dhambi ni mauti, lakini ni kweli pia kwamba wapo ambao wanapata ugonjwa huo bila wao kufanya chochote kile. “Mke yupo nyumbani, mme anachepuka na kuleta ukimwi nyumbani kwa mama… kama tukisema Ukimwi ni dhambi, huyo mama ana dhambi yake nini? Na mtoto aliyezaliwa na Ukimwi, tatizo la mtoto nini?” aliuliza Mkurugenzi akisisitiza haja ya kuondokana na unyanyapaa na kusaidia kwa pamoja kukabiliana na janga hilo. Unapotoa hotuba na kusema kwamba utakufa na Ukimwi wako, haitoi tumaini kwa mgonjwa na wewe unaweza kuwa sababu ya yeye kuamua kuambukiza watu zaidi alisema Mkurugenzi huyo. Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko akizungumza na washiriki wa mkutano wa kuimarisha uratibu wa Afua za Ukimwi katika Taasisi za Kidini uliofanyika Chuo cha Maendeleo na Uongozi wa Elimu (ADEM) Bagamoyo.
 “madhehebu yana nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko katika shughuli za Ukimwi” anasema Mkurugenzi na kuongeza kuwa yuko katika mapambano na Ukimwi kwa miaka 22 na ana kila sababu ya kusema kwamba madhehebu ya dini yana mchango mkubwa katika kampeni dhidi ya Ukimwi. Anasema akiwa mchungaji (alitolewa katika kazi hiyo) anaamini ipo haja ya kuwapo na mabadiliko ikiwa mapambano hayo yanatakiwa yafanikiwe. Mwakilishi wa UNESCO katika mkutano huo, Herman Mathias ambaye pia ni Mratibu wa Ukimwi Unesco akifafanua jambo wakati wa mkutano wa kuimarisha uratibu wa Afua za Ukimwi katika Taasisi za Kidini uliofanyika Chuo cha Maendeleo na Uongozi wa Elimu (ADEM) Bagamoyo uliofadhiliwa na UNESCO.
Katika mkutano huo ambao umefadhiliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) alisema kwa muda sasa imekuwa ukisimama na kutaja Ukimwi unaonekana kama umetaja dhambi hali ambayo inaongeza unyanyapaa na pia kuwafanya watu wasiwe wa wazi na afya zao. Aidha alisema kwamba kwa sasa kuna tatizo la wanaume wengi kutopima afya zao na hata wakipima hawafuati maelekezo na wanakuwa wa kwanza kufa kutokana na kushindwa kutumia dawa inavyotakiwa. Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mwitikio wa Kitaifa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Audrey Njelekela akizungumza kuhusu nafasi ya viongozi wa dini katika kuleta mabadiliko ya mapambano dhidi ya Ukimwi kwenye mkutano wa kuimarisha uratibu wa Afua za Ukimwi katika Taasisi za Kidini uliofanyika Chuo cha Maendeleo na Uongozi wa Elimu (ADEM) Bagamoyo kwa ufadhili wa UNESCO. Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa kuimarisha uratibu wa Afua za Ukimwi katika Taasisi za Kidini uliofanyika Chuo cha Maendeleo na Uongozi wa Elimu (ADEM) Bagamoyo kwa ufadhili wa UNESCO.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala “VIONGOZI WA DINI WASIKATISHE TAMAA WAUMINI KUKABILI UKIMWI”- DK. MABOKO

yaani makala yote “VIONGOZI WA DINI WASIKATISHE TAMAA WAUMINI KUKABILI UKIMWI”- DK. MABOKO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala “VIONGOZI WA DINI WASIKATISHE TAMAA WAUMINI KUKABILI UKIMWI”- DK. MABOKO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/viongozi-wa-dini-wasikatishe-tamaa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "“VIONGOZI WA DINI WASIKATISHE TAMAA WAUMINI KUKABILI UKIMWI”- DK. MABOKO"

Post a Comment