title : UKAGUZI MACHIMBO YA BUHEMBA KUKAMILIKA KABLA JANUARI 10, 2018
kiungo : UKAGUZI MACHIMBO YA BUHEMBA KUKAMILIKA KABLA JANUARI 10, 2018
UKAGUZI MACHIMBO YA BUHEMBA KUKAMILIKA KABLA JANUARI 10, 2018
Serikali imeagiza kufikia Januari 10, 2018 Ukaguzi wa Usalama kwenye eneo la Machimbo ya Dhahabu ya Buhemba, Wilayani Butiama Mkoani Mara uwe umekamilika ili shughuli za uchimbaji zilizokuwa zimesimamishwa ziruhusiwe.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo alitoa agizo hilo Desemba 27, 2017 alipofanya ziara kwenye eneo hilo ili kujionea hali halisi ya machimbo husika pamoja na kuzungumza na wachimbaji waliosimamishwa kuendeleza shughuli zao hadi hapo ukaguzi utakapokamilika.
“Ninasikitika kuona shughuli za uchumi kwenye eneo hili la Buhemba zimesimama kutokana na shughuli za uchimbaji kusimamishwa baada ya kutokea ajali,” alisema.
Serikali ilisitisha shughuli za uchimbaji Madini kwenye eneo hilo la Buhemba Februari 2017 baada ya kutokea vifo vya wachimbaji Watatu na wengine wapatao 15 kujeruhiwa kutokana na kufanya shughuli zao bila kuzingatia taratibu na kanuni za uchimbaji salama.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa tatu kutoka kushoto) akikagua moja ya shimo la dhahabu kwenye machimbo ya Buhemba.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi wakati wa ziara yake kwenye eneo la machimbo ya dhahabu la Buhemba, Wilayani Butiama, Mkoani Mara.
Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi (aliyesimama) akimkaribisha Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) kuzungumza na Wachimbaji (hawapo pichani). Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini (FEMATA), John Bina.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza na baadhi ya Wachimbaji kwenye Machimbo ya Dhahabu ya Buhemba.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala UKAGUZI MACHIMBO YA BUHEMBA KUKAMILIKA KABLA JANUARI 10, 2018
yaani makala yote UKAGUZI MACHIMBO YA BUHEMBA KUKAMILIKA KABLA JANUARI 10, 2018 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UKAGUZI MACHIMBO YA BUHEMBA KUKAMILIKA KABLA JANUARI 10, 2018 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/ukaguzi-machimbo-ya-buhemba-kukamilika.html
0 Response to "UKAGUZI MACHIMBO YA BUHEMBA KUKAMILIKA KABLA JANUARI 10, 2018"
Post a Comment