KITABU CHA KULETA MABADILIKO CHAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

KITABU CHA KULETA MABADILIKO CHAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KITABU CHA KULETA MABADILIKO CHAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KITABU CHA KULETA MABADILIKO CHAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM
kiungo : KITABU CHA KULETA MABADILIKO CHAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

soma pia


KITABU CHA KULETA MABADILIKO CHAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Kampuni ya Viva Legency inayohusika na mafunzo na ushauri elekezi imekuja na kitabu kinachojulikana kama "SOTE TUNAWEZA" kikiwa na lengo la kusaidia harakati za mabadiliko pamoja na kukuza utamaduni wa mtanzania.

Akizungumza  na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa Viva Legency Fortunata Temu amesema kuwa kitabu cha "SOTE TUNAWEZA" kimeandikwa kwa lugha ya kiswahili na kinampa msomaji uwezo mkubwa wa kubadili fikra na kupiga hatua ya kimaendeleo.

"Kitabu cha sote tunaweza kimeandikwa kwa lugha ya kiswahili na kinampa uwezo msomaji kubadili kifikra na kupiga hatua kiamaendeleo" amesema Fortunata.Amesema kuwa katika uandishi wa kitabu hicho wametumia mifano ya watu mbalimbali kutoka Tanzania na sehemu nyingine za dunia waliofanikiwa na kusema kuwa wametumia mifano hiyo ili kumtia hamasa msomaji na kumfanya kufuata nyendo za hao watu waliofanikiwa.

Fortunata ameongeza kuwa mafanikio yanaweza kupatikana kwa kuangalia fursa zinazopatikana ndani ya jamii hivyo kuwataka watanzania kutumia lugha ya kiswahili kama fursa kwa kuhabarishana na kuelimishana .Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia , Dk.Ave Maria Semakafu ameipongeza kampuni ya Vivalegency na kusema kuwa kitabu cha "SOTE TUNAWEZA" kimekuja wakati mwafaka kwa sababu nchi yetu ipo kwenye harakati za mabadiliko kuelekea uchumi wa kati.

"Sote tunaweza kimekuja wakati mwafaka kwa sababu nchi yetu ipo kwenye harakati za mabadiliko kuelekea uchumi wa kati" amesema Dk.Semakafu.

Amesema Tanzania inachangamoto kubwa katika utamaduni wa uandishi na usomaji vitabu na kuwaomba watanzania watumie fursa ya kuandika vitabu vyenye dhima yenye kuleta maana na kuachana na utamaduni wa kuandika vitabu ambavyo havina dhima yoyote ya kubadili fikra na kuleta chachu ya maendeleo.
 Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Viva Legacy (T) Bi. Fortunata Meela Temu akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi wa kitabu chaake cha "SOTE TUNAWEZA" leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Dkt. Avemaria Semakafu na Mwajiri Msaidizi wa Viva Legacy (T) Ltd Bi. Neema Seleman.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Avemaria Semakafu (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi wa kitabu chaake cha "SOTE TUNAWEZA" leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus, na Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa VIVA lEGACY lTD (t) Bi. Fortunata Meela Temu.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Stadi Dkt. Avemaria Semakafu (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Viva Legacy Ltd (T) Bi. Fortunata Meela Temu wakiwaonyesha Waandishi wa Habari kitabu cha "SOTE TUNAWEZA"  leo Jijini Dar es Salaam. Kitabu hicho kimetungwa kwa lengo la kuimarisha mfumo wa utendaji na hasa kuboresha rasilimali watu. 
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano baina yao na  na Mkurugenzi wa Viva Legacy (T) Ltd  alipokuwa akizungumzia kuhusu uzinduzi wa kitabu cha SOTE TUNAWEZA leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na: Frank Shija - MAELEZO)


Hivyo makala KITABU CHA KULETA MABADILIKO CHAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

yaani makala yote KITABU CHA KULETA MABADILIKO CHAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KITABU CHA KULETA MABADILIKO CHAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/kitabu-cha-kuleta-mabadiliko.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KITABU CHA KULETA MABADILIKO CHAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM"

Post a Comment