title : Kila la Kheri Zanzibar Heroes
kiungo : Kila la Kheri Zanzibar Heroes
Kila la Kheri Zanzibar Heroes
Timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes leo inaingia dimbani kupambana na wenyeji Kenya katika mashindano ya Chalenji yanayoendelea nchini Kenya.
Blog ya ZanziNews inaitakia kila la kheri timu yetu ili na leo iibuke na ushindi kama ilivyoweza kushinda katika michezo miwili iliyopita na kujiweka katika mazingira mazuri ya kucheza nusu fainali.
Ikumbukwe kwamba Timu yetu imeweza kushiriki katika mashindano haya licha ya kuwa na maandalizi duni, kwani hata safari ya kwenda nchini Kenya ilikuwa ni ya kuungaunga tu kwa usafiri wa mabasi hadi kuwasili Machakos.
Hata hivyo ari kubwa waliyoonesha vijana wetu licha ya changamoto, licha ya kutokuwa na majina makubwa lakini soka wanalitendea haki kwa uthibitisho wa michezo yote waliyoibuka washindi hawakubahatisha bali walistahiki.
Na leo macho yetu yatakuwa mjini Machakos kuitakia ushindi mwengine dhidi ya miamba ya Harambee stars kwani wazungu wana msemo The bigger they are, The harder they fall.
Tuiombee dua kwa wingi timu yetu iibuke na ushindi leo
Go Zanzibar Heroes Go!
Hivyo makala Kila la Kheri Zanzibar Heroes
yaani makala yote Kila la Kheri Zanzibar Heroes Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Kila la Kheri Zanzibar Heroes mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/kila-la-kheri-zanzibar-heroes.html
0 Response to "Kila la Kheri Zanzibar Heroes"
Post a Comment