title : DK MNDOLWA KULIPA MADENI YA WATENDAJI JUMUIYA YA WAZAZI NDANI YA SIKU 100 [19:04, 12/23/2017] Yassir:
kiungo : DK MNDOLWA KULIPA MADENI YA WATENDAJI JUMUIYA YA WAZAZI NDANI YA SIKU 100 [19:04, 12/23/2017] Yassir:
DK MNDOLWA KULIPA MADENI YA WATENDAJI JUMUIYA YA WAZAZI NDANI YA SIKU 100 [19:04, 12/23/2017] Yassir:
Na Said Mwinshehe-Globu ya Jamii.
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Dk.Edmund Mndolwa amesema ndani ya siku 100 kuanzia jana atahakikisha analipa madeni yote wanayodai watendaki wa jumuiya hiyo huku akitoa onyo kwa wale wenye tabia ya kutengeneza makundi.
Amesema hayo wakati anazungumza na Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kumpokea rasmi ambapo amesisitiza kusimamia vema majukumu yake kwa maslahi ya jumuiya na CCM kwa ujumla.
Kuhusu madeni,amesema anatambua changamoto zilizopo ikiwamo ya watendaji wa ngazi mbalimbali kudai fedha zao lakini hilo atalishughulikia ndani ya siku 100 kwani fedha zipo."Najua changamoto zilizopo kwenye jumuiya yetu,nitumie nafasi kuwahakikishia watendaji wanaodai ndani ya siku 100 tutalipa madeni yote.
" Nitaboresha maslahi na kubwa zaidi tutanunua vitendea kazi kwani vilivyopo vimechakaa na viachache.Lengo na kuifanya jumuiya yetu kutimiza majukunu yake na tutaendelea kujiimarisha hatua kwa hatua,"amesema.Ametumia nafasi hiyo kuelezea kusikitishwa kwake na tabia ya uwepo wa makundi ambayo kimsingi hayana nia njema zaidi ya kukiharibu chama chao ,hivyo lazima wakomeshe makundi .
"Atakayebainika anajihusisha na makundi atachukuliwa hatua,sisi ni wamoja na lazima tusimame katika hilo.Chaguzi zimekwisha ndani ya jumuiya ,sasa tufanye kazi," amesema Dk.Mndolwa.Ametoa onyo kuhusu tabia ya watu kuwa na tabia ya kuzungumzia mambo ya jumuiya na chama bila kufuata utaratibu.
Hivyo amesema lazima anayetaka kuzungumza basi ahakikishe anatumia vikao halali ambapo atajenga hoja na kusikilizwa."Atakayezungumza bila kufuata utaratibu hatutamuacha,lazima kanuni na taratibu ziheshimiwe na kila mmoja wetu,"amesisitiza.
Hivyo makala DK MNDOLWA KULIPA MADENI YA WATENDAJI JUMUIYA YA WAZAZI NDANI YA SIKU 100 [19:04, 12/23/2017] Yassir:
yaani makala yote DK MNDOLWA KULIPA MADENI YA WATENDAJI JUMUIYA YA WAZAZI NDANI YA SIKU 100 [19:04, 12/23/2017] Yassir: Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DK MNDOLWA KULIPA MADENI YA WATENDAJI JUMUIYA YA WAZAZI NDANI YA SIKU 100 [19:04, 12/23/2017] Yassir: mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/dk-mndolwa-kulipa-madeni-ya-watendaji.html
0 Response to "DK MNDOLWA KULIPA MADENI YA WATENDAJI JUMUIYA YA WAZAZI NDANI YA SIKU 100 [19:04, 12/23/2017] Yassir:"
Post a Comment