TINGATINGA LABOMOA MAJENGO YA WIZARA YA MAJI

TINGATINGA LABOMOA MAJENGO YA WIZARA YA MAJI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TINGATINGA LABOMOA MAJENGO YA WIZARA YA MAJI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TINGATINGA LABOMOA MAJENGO YA WIZARA YA MAJI
kiungo : TINGATINGA LABOMOA MAJENGO YA WIZARA YA MAJI

soma pia


TINGATINGA LABOMOA MAJENGO YA WIZARA YA MAJI

TINGATINGA limeanza kubomoa majengo ya Wizara ya Maji yaliyopo eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam kufuatia amri ya Rais John Magufuli aliyoitoa hivi karibuni.

Jengo lingine ambalo lkinatarajia kubomolewa na tingatinga ni la Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), ambalo linatazamana na wizara ya maji eneo la Ubungo.

Majengo hayo yanatakiwa kubomolewa ili kupisha ujenzi wa barabara itakayoanzia Ubungo hadi Chalinze mkoani Pwani kwa njia sita.

Leo asubuhi majengo hayo ya wizara yameanza ‘kupigwa nyundo’ ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli ambaye aliagiza majengo ya wizara hiyo na ghorofa la Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuwekwa alama ya X kwa ajili ya kubomolewa.

Novemba 15,2017 akitokea Chato alipokwenda kwa mapumziko baada ya ziara ya Uganda, Rais Magufuli aliagiza Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kuweka alama ya X katika jengo la Tanesco na Wizara ya Maji, sehemu zilizo katika hifadhi ya barabara.

Katika majengo ya Wizara ya Maji, tingatinga limevunja ukuta, huku watu wengine wakiendelea na kazi ya kuondoa madirisha na milango kwenye majengo. Jengo lililoanza kubomolewa ni la ofisi ya Waziri wa Maji.

Wafanyakazi wa wizara hiyo wanaendelea kutoa mali ndani ya majengo waliyokuwa wakiyatumia kwa ofisi.

Mbali ya majengo hayo, Tanraods inaendelea kuweka alama ya X kwenye nyumba za wananchi zilizo katika hifadhi ya barabara ikiwa ni pamoja na kupisha ujenzi wa barabara za juu eneo la Ubungo.

Tayari nyumba takriban 1,200 zikiwamo tano za ibada, vituo vya mafuta na baa katika eneo la Ubungo hadi Kimara mwisho zimewekwa alama kwa ajili ya ubomoaji.

Kwa mujibu wa Tanroads, ubomoaji katika eneo la Ubungo hadi Kimara mwisho unahusisha nyumba zilizo mita 91.7 katika hifadhi ya barabara ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya Hifadhi ya Barabara ya mwaka 1932.


Hivyo makala TINGATINGA LABOMOA MAJENGO YA WIZARA YA MAJI

yaani makala yote TINGATINGA LABOMOA MAJENGO YA WIZARA YA MAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TINGATINGA LABOMOA MAJENGO YA WIZARA YA MAJI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/tingatinga-labomoa-majengo-ya-wizara-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TINGATINGA LABOMOA MAJENGO YA WIZARA YA MAJI"

Post a Comment