title : NEC yakiridhia kuhamishwa vituo 21 vya kupigia kura Mbweni
kiungo : NEC yakiridhia kuhamishwa vituo 21 vya kupigia kura Mbweni
NEC yakiridhia kuhamishwa vituo 21 vya kupigia kura Mbweni
Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani akiwa na kitabu cha wageni kwenye Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Malindi Estate ambayo ipo kwenye nyumba ya mmoja wa wagombea wa Uchaguzi Mdogo wa Madiwani Kata ya Mbweni. Picha na NEC.
Hussein Makame-NEC
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imejiridhisha kuwa uamuzi wa kuvihamisha vituo 21 vya kupigia kura katika Kata ya Mbweni, jimbo la Kawe katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, umezingatia Sheria na Kanuni za Uchaguzi.
NEC imetoa msimamo huo, baada ya kupokea taarifa kutoka kwa baadhi ya wananchi na vyama vya siasa wakilalamika kuwa Tume ya uchaguzi imehamisha vituo vinane (8) vya kupigia kura na kuvipeleka kwenye Kituo cha Polisi, hatua waliyoeleza kuwa ni kuwanyima haki wapiga kura katika kutimiza haki ya msingi.
Malalamiko mengine yaliyoifikia NEC ni kwamba Tume ilivihamisha vituo vingine 15 kutoka maeneo ya awali na kuvipeleka maeneo mengine jambo ambalo baadhi ya vyama havikukubaliana na uamuzi huo.
Kutokana na malalamiko hayo, jana Jumanne Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Kailima Ramadhani akiambatana na watendaji wengine wa Tume, walitembelea maeneo hayo na kujiridhisha kuwa mabadiliiko ya vituo yaliyofanywa na msimamizi wa uchaguzi yamekidhi matakwa ya kisheria.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Hivyo makala NEC yakiridhia kuhamishwa vituo 21 vya kupigia kura Mbweni
yaani makala yote NEC yakiridhia kuhamishwa vituo 21 vya kupigia kura Mbweni Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NEC yakiridhia kuhamishwa vituo 21 vya kupigia kura Mbweni mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/nec-yakiridhia-kuhamishwa-vituo-21-vya.html
0 Response to "NEC yakiridhia kuhamishwa vituo 21 vya kupigia kura Mbweni"
Post a Comment