title : NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MARY MWANJELWA ASEMA MPANGO WA SERIKALI KUPELEKA MBEGU MPYA ZA KAHAWA WILAYANI MBINGA NI KUINUA UZALISHAJI
kiungo : NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MARY MWANJELWA ASEMA MPANGO WA SERIKALI KUPELEKA MBEGU MPYA ZA KAHAWA WILAYANI MBINGA NI KUINUA UZALISHAJI
NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MARY MWANJELWA ASEMA MPANGO WA SERIKALI KUPELEKA MBEGU MPYA ZA KAHAWA WILAYANI MBINGA NI KUINUA UZALISHAJI
Na Mathias Canal, Dodoma
Serikali imesema kuwa Mpango wa Serikali wa kuwapelekea wakulima wa Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma mbegu mpya za Kahawa ni mahususi kwa ajili ya kuinua uzalishaji kwa kutekeleza Mpango Mkakati wa Kuendeleza Zao la Kahawa katika kipindi cha miaka 10 yaani mwaka (2011 – 2021).
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Machuche Mwanjelwa (Mb) amebainisha hayo leo Novemba 10, 2017 Bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mhe Martin Mtonda Msuha (Mb) Aliyetaka kufahamu kuhusu kushuka Kwa takwimu katika miaka ya hivi karibuni ya uzalishaji wa Kahawa Wilayani Mbinga kwa mkulima mmoja mmoja (out growers) ambapo alitaja sababu za mojawapo zilizopelekea kushuka kwa uzalishaji huo kuwa ni pamoja na kuzeeka kwa miti ya kahawa.
Mhe Mwanjelwa alisema kuwa Katika mpango huo, utafiti na usambazaji wa miche bora itatolewa ili kuondokana na miche yenye tija duni na iliyozeeka. Ambapo Utekelezaji wake unafanyika kwa kushirikiana na wadau hususani Tanzania Coffee Research Institute (TaCRI).
Alisema, Kituo cha Utafiti na uzalishaji miche cha Ugano kilichopo Wilayani Mbinga, katika mwaka 2016/2017 kilizalisha na kusambaza miche bora ya kahawa 270,869 na kazi mpaka hivi sasa inaendelea.
Aidha, Mfuko wa Maendeleo ya Kahawa (Tanzania Coffee Developemnt Fund (TCDF) umefadhili na kupunguza bei kutoka shilingi 300 kwa mche mmoja hadi shilingi 150 kwa vituo vyote nchini vilivyoko chini ya TaCRI ili miche hiyo isambae kwa kasi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Machuche Mwanjelwa (Mb) akijibu maswali Bungeni Mjini Dodoma Leo Novemba 10, 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Machuche Mwanjelwa (Mb) akijadili jambo na Mhe Jenista Joakim Mhagama ambaye ni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu.
Hivyo makala NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MARY MWANJELWA ASEMA MPANGO WA SERIKALI KUPELEKA MBEGU MPYA ZA KAHAWA WILAYANI MBINGA NI KUINUA UZALISHAJI
yaani makala yote NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MARY MWANJELWA ASEMA MPANGO WA SERIKALI KUPELEKA MBEGU MPYA ZA KAHAWA WILAYANI MBINGA NI KUINUA UZALISHAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MARY MWANJELWA ASEMA MPANGO WA SERIKALI KUPELEKA MBEGU MPYA ZA KAHAWA WILAYANI MBINGA NI KUINUA UZALISHAJI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/naibu-waziri-wa-kilimo-mhe-mary_10.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MARY MWANJELWA ASEMA MPANGO WA SERIKALI KUPELEKA MBEGU MPYA ZA KAHAWA WILAYANI MBINGA NI KUINUA UZALISHAJI"
Post a Comment