Abiria wa vivuko vya Kigamboni na Magogoni wapewa elimu namna ya kujiokoa

Abiria wa vivuko vya Kigamboni na Magogoni wapewa elimu namna ya kujiokoa - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Abiria wa vivuko vya Kigamboni na Magogoni wapewa elimu namna ya kujiokoa, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Abiria wa vivuko vya Kigamboni na Magogoni wapewa elimu namna ya kujiokoa
kiungo : Abiria wa vivuko vya Kigamboni na Magogoni wapewa elimu namna ya kujiokoa

soma pia


Abiria wa vivuko vya Kigamboni na Magogoni wapewa elimu namna ya kujiokoa

Mwambawahabari
Wanafunzi kutoka chuo cha Bahari nchini (DMI) wamefanya zoezi la kufundisha abiria wanaotumia
kivuko cha Magogoni Kigamboni jinsi ya kutumia vifaa vya kujiokolea vilivyomo katika vivuko hivyo pindi inapotokea dharura ya ajali kwenye maji.

Zoezi hilo lililoratibiwa na chuo cha Bahari kwa kushirikiana na kitengo cha Habari na Mawasiliano
(TEMESA) limefanyika kivukoni hapo mapema asubuhi likiongozwa na Nahodha Nyamurasa Matage
kutoka chuo hicho. Zoezi hilo lilihusisha wanafunzi wa kozi ya PST na lilikua na nia ya kuwaonyesha
watumiaji wa kivuko hicho namna ya kujiokoa na pia kujifunza kuwa na utulivu pindi inapotokea dharura ya ajali, moto au kuzimika kwa kivuko.

Akizungumza katika tukio hilo Nahodha Nyamurasa aliwataka watumiaji wa kivuko hicho kuhakikisha
wanafuatilia kwa makini zoezi hilo kwani dharura ya ajali inaweza kutokea wakati wowote na mahala
popote hivyo abiria wanatakiwa kuwa watulivu pindi inapotokea. Alisema mafunzo hayo yalikua ni
sehemu ya masomo yao ya darasani lakini pia elimu tosha kwa watumiaji wa vivuko.

Naye Mkuu wa kivuko Magogoni Kigamboni Mhandisi Lukombe King’ombe akizungumza wakati wa zoezi hilo aliwataka wanafunzi hao kulichukulia kwa umakini zoezi hilo kwani pindi wanapomaliza mafunzo yao wanatumiwa katika vivuko vya TEMESA katika shughuli za uokoaji wa abiria na mali zao na pia kutoa maelekezo ya usalama kwa abiria wa vivuko hivyo.

“Hili ni zoezi muhimu kwa abiria wetu kulipata na kujifunza namna ya kutumia vifaa vya kujiokolea ambavyo vinakuwepo muda wote katika vivuko vyetu,” alisema King’ombe.

Dhumuni kubwa la zoezi hilo lilikua ni kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa Chuo hicho na pia kutoa
mafunzo kwa abiria wanaotumia kivuko. Zoezi hilo linategemewa kuendelea wiki ijayo katika kivuko
hicho.



Hivyo makala Abiria wa vivuko vya Kigamboni na Magogoni wapewa elimu namna ya kujiokoa

yaani makala yote Abiria wa vivuko vya Kigamboni na Magogoni wapewa elimu namna ya kujiokoa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Abiria wa vivuko vya Kigamboni na Magogoni wapewa elimu namna ya kujiokoa mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/abiria-wa-vivuko-vya-kigamboni-na.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Abiria wa vivuko vya Kigamboni na Magogoni wapewa elimu namna ya kujiokoa"

Post a Comment