SETH ASIPTIBIWA HARAKA ANAWEZA KUFARIKI...... PUTO LIMEISHA MUDA WAKE

SETH ASIPTIBIWA HARAKA ANAWEZA KUFARIKI...... PUTO LIMEISHA MUDA WAKE - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SETH ASIPTIBIWA HARAKA ANAWEZA KUFARIKI...... PUTO LIMEISHA MUDA WAKE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SETH ASIPTIBIWA HARAKA ANAWEZA KUFARIKI...... PUTO LIMEISHA MUDA WAKE
kiungo : SETH ASIPTIBIWA HARAKA ANAWEZA KUFARIKI...... PUTO LIMEISHA MUDA WAKE

soma pia


SETH ASIPTIBIWA HARAKA ANAWEZA KUFARIKI...... PUTO LIMEISHA MUDA WAKE

MSHTAKIWA wa makosa ya uhujumu Uchumi, Harbinder Singh Sethi ambaye ni mmiliki wa IPTL, ameileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa 'Puto-Balloon' alilowekewa tumbon limeisha muda wake (expire) na asipobadilishwa litamsababishia kifo.

Wakili wa Seth, Alex Balomi mbele ameileza hayo leo Octoba 27 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Mwendesha Mashtaka kutoka Takukuru, Leornad Swai kueleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba kesi iahirishwe.

Katika kesi hiyo Sethi anashtakiwa  pamoja na mmiliki mwenza, James Rugemarila ambapo wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka  12 ya  uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

Akielezea kuhusu matibabu ya Sethi, wakili Balomi amedai, pamoja na kutekelezwa kwa amri ya mahakama ya kuamuru mshtakiwa akatibiwe Muhimbili, ambapo alipelekwa na kufanyiwa vipimo lakini mpaka leo hajapatiwa majibu ya vipimo wala matibabu.

Amedai kuwa Puto lililowekwa tumboni kwa mshytakiwa limeisha muda wake, na  linatakiwa kubadilishwa mwishoni mwa mwezi huu wa Octoba

"Kama hilo balloon halitabadilishwa linaweza kugeuka sumu na kuondoa uhai wake, hivyo daktari aliyechukua vipimo anapaswa kumpatia majibu,". Alidai

Kufuatia hali hiyo ya mteja wake, ameomba upande wa mashtaka ukamilishe upelelezi kwani  watuhumiwa wanateseka jela bila sababu huku

Akijibu hoja hizo, Wakili Swai amedai mshtakiwa Seth alipelekwa hospital Octoba 13 mwaka huu na kufanyiwa vipimo na daktari, lakini majibu yake ni siri ya Daktari na mshtakiwa na sio vya kuongelea mahakamani.

Alidai kuwa kuhusu upelelezi wanaendelea kufanyia kazi.

Baada ya hayo yote, Hakimu Shaidi amesema mahakama ilitoa amri kwamba Seth apelekwe hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu na amepelekwa, hivyo daktari amekamilisha kazi yake,  mawakili wanaweza kwenda kuulizia kuhusu vipimo vyake huko Hospitali

Aidha ameuagiza upande wa mashtaka kuhakikisha upelelezi unakamilika mapema. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 10 mwaka huu.


Hivyo makala SETH ASIPTIBIWA HARAKA ANAWEZA KUFARIKI...... PUTO LIMEISHA MUDA WAKE

yaani makala yote SETH ASIPTIBIWA HARAKA ANAWEZA KUFARIKI...... PUTO LIMEISHA MUDA WAKE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SETH ASIPTIBIWA HARAKA ANAWEZA KUFARIKI...... PUTO LIMEISHA MUDA WAKE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/seth-asiptibiwa-haraka-anaweza-kufariki.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SETH ASIPTIBIWA HARAKA ANAWEZA KUFARIKI...... PUTO LIMEISHA MUDA WAKE"

Post a Comment