MAONI YA MDAU: UCHUMI WA VIWANDA

MAONI YA MDAU: UCHUMI WA VIWANDA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAONI YA MDAU: UCHUMI WA VIWANDA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAONI YA MDAU: UCHUMI WA VIWANDA
kiungo : MAONI YA MDAU: UCHUMI WA VIWANDA

soma pia


MAONI YA MDAU: UCHUMI WA VIWANDA

Naunga mkono harakati za kuwa na Uchumi wa Viwanda.

Wakati wa Ukoloni, mataifa ya Afrika yalikuwa ni wazalishaji wa mali-ghafi wa viwanda vya watawala wao. Baada ya Afrika kujikomboa, Afrika ilianza harakati za kujikomboa ki uchumi. Na mataifa mengi yalijenga viwanda vya kila bidhaa muhimu.
 Kuanzia miaka ya tisini, mataifa mengi ya Afrika yaliingia katika Uchumi huria ulioambatana na vyama vingi vya kisiasa. Uchumi huru ulileta changamoto nyingi hasa kwa viwanda vingi vya ndani. Uchumi guru ulikuja na bidhaa bora, nzuri na za aina tofauti tofauti.

Viwanda vya ndani vilishindwa kuhilimili mikikimiki ya ushindani, ukichanganya na utawala na usimamizi mbovu, ufisadi, na hujuma viwanda vingi vilikufa. Kuanzia miaka hiyo ya tisini mwishoni na miaka ya elfu mbili na kuendelea, Afrika imekuwa ikipokea kila aina ya bidhaa kutoka nje ya bara hili, ziwe bidhaa mpya au mitumba.

Kilichonisukuma kuandika ni baada ya kuhudhuria mhadhara kuhusu kupiga marufuku mitumba kwa mantiki ya kutengeneza chachu ya kufufua viwanda vyetu hasa hasa viwanda vya nguo na viatu, ikizingatiwa Tanzania tunazalisha pamba na ngozi. Hapo awali, mitumba ilikuwa ni ya nguo na viatu tu. Leo hii kuna mitumba ya kila aina. Mitumba ya nguo, viatu, magari, bidhaa za majumbani, ndege, meli,baisikeli,vifaa vya maosipitalini,mashuleni nakadhalika. Tuna mitumba hadi ya Wataalamu.
Nia yangu sio kuongelea aina za mitumba inayoingia Afrika na Tanzania ikiwepo. Nia yangu ni kujaribu kuona ni namna gani hii mitumba inaweza kuisadia Afrika hasa hasa Tanzania katika hii Sera ya Uchumi wa viwanda. Kwa muda mrefu, Afrikaimelalamika kuwa jalala la bidhaa chakavu na kukuuu kutoka nje. Mbinu nyingi zimefanyika kuzuia uingizwaji wa bidhaa chakavu,kukuu na zilizo chini ya kiwango, aidha kwa kuzitoza kodi kubwa au kwa kuzipiga marufuku.

Pia viongozi wa Kisiasa wamejeribu Mara nyingi kukataa uingizwaji wa mitumba katika mataifa yao ya Afrika. Hivi karibuni tulishuhudia jumuiya ya Afrika Mashariki ikiazimia hadi ifikapo mwaka 2019 iwe mwisho wa kuingiza mitumba katika jumuiya.

Dalili za kushindikana kwa azma hii zishaanza kuonekana kwa majirani zetu Kenya kushinikizwa hadi kujitoa katika mpango huo. Hivyo basi mbinu pekee inayobaki ni Afrika kuwa na viwanda vyake vitakavyozalisha bidhaa kwa ajili ya kukidhi mahitaji yao ya ndani. Tatizo litabaki kwenye ushindani.

Mimi siungi mkono hoja ya kupiga marufuku MITUMBA na siungi mkono hoja ya kuwekeza katika viwanda vitakavyodhalisha bidhaa kama za nje halafu tuhimizane kuwa na UZALENDO katika kutumia bidhaa zetu.

Nashauri tujenge VIWANDA vitakavyo RECYCLE MITUMBA ya kila aina, iwe nguo, viatu,magari,vifaa vya kielektroniki na kadhalika. so called conflict of interest 

Baada ya KU RECYCLE, tuwauzie tena wazungu malighafi.  Hapa na maanisha kwamba TU SI RECYCLE hadi kuzalisha bidhaa, bali tuichakate MITUMBA iwe tena malighafi.

Kwa sisi kuwa na viwanda vya aina hii tutaepusha the so called conflict of interest na tutakuwa unique katika aina ya viwanda tulivyonavyo.

Theophani C. Ishika
Assistant Lecturer
CFR.


Hivyo makala MAONI YA MDAU: UCHUMI WA VIWANDA

yaani makala yote MAONI YA MDAU: UCHUMI WA VIWANDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAONI YA MDAU: UCHUMI WA VIWANDA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/maoni-ya-mdau-uchumi-wa-viwanda.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAONI YA MDAU: UCHUMI WA VIWANDA"

Post a Comment